Mshindi
wa Shindano la Redd’s Miss Ukonga 2013, Martha Gewe (katikati) akiwa
katika picha ya pamoja na mshindi wa pili, Diana Joachim (kushoto)
pamoja na mrembo aliyeshika nafasi ya tatu, Natasha Mohamed mara baada
ya warembo hao kutangazwa kuwa ndio washindi wa shindano hilo Usiku wa
kuamkia jana katika shindano lililofanyika Ukumbi wa Wenge Garden Ukonga
Mombasa jijini Dar es Salaam. Martha aliwashinda warembo wengine 12
katika shindano hilo.
Warembo
waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora ya Redd’s Miss Ukonga 2013
wakiwa katika picha ya pamoja kutoka kushoto ni Vanesa Magile, Matha
Gewe, Diana Joachim, Natasha Mohamed na Nancy Abasy shindano lilifanyika
Ukumbi wa Wenge Garden Ukonga Mombasa jijini Dar es Salaam. Martha.
Baadhi
ya washiriki wa Shindano la Redd’s Miss Ukonga 2013 wakicheza show ya
ufunguzi wa shindano lao lililofanyika usiku wa kuamkia jana katika
ukumbi wa Wenge Garden Ukonga jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment