JUMLA
ya Warembo 16 wa Kanda ya Temeke, wameanza kujinoa jana (Juni 17)
kwenye klabu ya TCC Chang'ombe, tayari kwa kinyanga'nyiro
kitakochafanyika Julai 5, mwaka huu katika ukumbi huo.
Idadi
hiyo ya warembo ni kutoka Kigamboni, Kurasini na Chang'ombe ambao
wanawania taji linaloshikiliwa na Miss Tanzania namba tatu, Edda
Sylvester ambaye atakuwa mmoja wa wakufunzi katika kambi hiyo, ambayo
pia inasimamiwa na Suzy Mwenda na Shadya Mohamed.
Mbali
ya hao, pia kutakuwa na jopo na wakufunzi wa dansi, litakaloongozwa na
Bokilo na Charles yote katika kuhakikisha shoo ya mwaka huu, itaendana
na ubora wa warembo wanaoshiriki shindano hilo, ambapo kwa hakika Redds
Miss Tanzania mwaka huu, bila shaka atatokea katika kanda hiyo, yenye
historia ya mafanikio.
Temeke,
imewahi kutoa warembo kadhaa miaka ya nyuma waliopata mafanikio katika
mashindano hayo, mitindo na kazi nyingine hasa kupata uzoefu wa
kujiamini katika njanja mbalimbali.
Miongoni
mwao ni Miriam Odemba(1997) aliyepata kuiwakilisha Tanzani katika
fainali za mitindo zilizofanyika Nice Ufaransa na kupata mkataba wa
Elite Model Look, baadaye kufakinikiwa kutwaa nafasi ya pili ya Miss
Earth World, zilizofanyika China.
Pia,
Temeke ilimtoa Happines Millen Magesse(2001), na kutwaa taji la Miss
Tanzania na kwa sasa anang'ara sana katika tasnia ya mitindo katika nchi
za Marekani, Afrika Kusini na barani Afrika kwa ujumla. 2003 Temeke
ilimtoa Miss Tanzania, Sylvia Bahame na 2006 kuwatoa Jokate Mwegelo na
Irene Uwoya.
Jokate
alitwaa taji la Miss Temeke mwaka huu na pia kushika nafasi ya pili
Miss Tanzania na pia kushinda taji la ubalozi wa Redd's na gazeti la
Citizen. Uwoya ambaye alikuwa mshindi wa pili Temeke alishika nafasi ya
nne kwenye Miss Tanzania mwaka huo. Genevieve Mpangala mwaka 2010
alitwaa taji la Miss Temeke baadaye kushinda taji la Miss Tanzania.
Nafasi
nyingine za juu zilizowahi kutwaliwa na warembo kutoka Temeke ni pamoja
na Irene Kiwia, mshindi wa nne Miss Tanzania mwaka 2000, Regina Mosha
mshindi wa nne Miss Tanzania mwaka 2002, Cecylia Assey mshindi wa pili
Miss Tanzania 2004, Queen David mshindi wa tatu mwaka 2007 na Edda
Sylvester mshindi wa tatu Miss Tanzania akiwa anashikilia taji la Redds
Miss Temeke.
Shindano
hilo, linalotarajiwa kuwa na burudani ya kipekee limedhaminiwa na
kinywaji cha Redd's, Dodoma Wine, Jambo Leo, Blogu ya Wananchi (Le
Mutuz), Fredito Entertainment, Kitwe General Traders na CXC Africa tours
& Safaris.
Warembo wa Redds Miss Temeke 2013
1-Axsaritha Vedastus
2-Belinda Paul
3-Darling Mmary
4-Esther Muswa
5-Hyness Oscar
6-Irene Rajab
7-Jamila Thomas
8-Latifa Mohamed
9-Margreth Gerald
19-Margreth Olotu
11-Mey Karume
12-Mutesi George
13-Naima Ramadhan
14-Narietha Boniface
15-Stella Mngazija
16-Svtlona Nyameyo
0 comments:
Post a Comment