Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukandara akinzungumza na wanahabari mchana juu jijini Dar es Salaam ofisini kwake
Wanahabari wakimsikiliza waziri Mukandara
Mpiga picha mkuu wa Jambo leo na kamanda wa matukio Richard Mwaikenda kulia akitafakari swali na kumuuliza waziri
..................................................................
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukandara
azungumza na wanahabari mchana huu ikiwa ni pamoja na kueleza
mafanikio ambayo serikali ya Rais Jakaya Kikwete imeyapata katika
ziara yake na Rais nchini Uingereza.
Mbali ya kueleza kusudio la wahisani wa klabu ya Sanderland kuja kujenga Academy ya mpira wa miguu kupitia kampuni ya Symbion Power ya Marekani nchini Tanzania kama njia ya kukuza michezo hapa nchini bado amesema kuwa ujenzi wa Academi hiyo utafanyika ndani ya jiji la Dar es Salaam ama Kibaha na kumpongeza mbunge wa jimbo la Ilala ambae alianza jitihada za kuomba msaada huo .
Pia waziri huyo amewataka wabunge nchini kuendelea kupigania ujenzi wa viwanja vya michezo katika maeneo yao pamoja na kuiga mfano wa mbunge wa jimbo la Ilala mhe. Zungu katika kuwawezesha kupata viwanja vya kidongo chekundu
Kuhusu mchezo kati ya Taifa Stars Ivory Coast waziri huyo alisema
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UJENZI WA ACADEMY YA MPIRA WA MIGUU HAPA NCHINI
§ Kama
mnavyofahamu, hivi karibuni Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania
alikuwa katika ziara yake ya kikazi nchini Uingereza.
§ Mhe.
Rais alipokuwa nchini Uingereza alitembelea Club ya Sunderland.
Mhe. Rais alihahidiwa kujengewa
Academy ya Mpira wa Miguu
na Kampuni ya Symbion Power ya Marekani ambayo itashirikiana na Club ya
Sanderland katika kuindesha.
§ Hiyo Academy tunategemea
itawezesha clubs zetu kupata wachezaji walio bora na walioandaliwa kuwa
wachezaji wa taifa na kimataifa na hivyo kuboresha timu yetu ya Taifa na
kuendelea kukuza muamuko wa masuala ya mpira wa miguu nchini.
§ Tunatarajia
suala hili litafanyika na kutekelezwa mapema iwezekanavyo
§ Katika mpango huo,
Kampuni ya Symbion pia itajenga viwanja vya michezo (sports courts) pale
Kidongo Chekundu.
§ Kutokana na umuhimu wa suala hili, viongozi wakuu wa
Kampuni ya Symbion wanatarajia kuja hapa nchini na nitakutana nao kwa ajili ya makubaliano
mbalimbali na maandalizi ya utekelezaji.
§ Hivi sasa kama Serikali tunatafuta sehemu itakayojengwa
Academy hiyo.
§ Matarajio au nia yetu ni kujenga Academy hiyo Dar es
Salaam au maeneo yaliyo karibu na Dar es Salaam.
§ Napenda nichukue fursa hii kumshukuru sana Mh. Rais kwa
kufanikisha suala hili.
§ Napenda pia
kumshukuru Mbunge wa Ilala Mhe. Mussa Zungu Azzan kwa kuwezesha kupatikana kwa
viwanja vya Kidongo Chekundu.
§ Napenda pia kutumia fursa hii kuwapongeza na kuwashukuru
vijana wetu wa timu ya Taifa ”Taifa Stars” kwa juhudi na mchezo mzuri
waliouonyesha wakati wa mechi yao na Timu ya Taifa ya Ivory Coast jumapili
iliyopita. Tupo pamoja nao na
tutaendelea kuhakikisha tunawajengea uwezo zaidi ili waweze kupata mafanikio
makubwa huko mbeleni.
§ Huko tunakoelekea, Academy itakuwa chimbuko la kupata
wachezaji wazuri wa timu ya Taifa.
Asanteni kwa
kunisikiliza
Picha na Francis Godwin
0 comments:
Post a Comment