ASKARI Polisi wa
Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Ramadhan Seleman (27), mkazi wa jijini Dar es
Salaam, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es
Salaam, akikabiliwa na shtaka la kukutwa na meno ya tembo yenye thamani ya Sh milioni
121. Askari huyo amefikishwa mahakamani, ikiwa ni wiki mbili tangu Ofisa Uvuvi
wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Seleman Chasama afikishwe mahakamani kwa
tuhuma za kukutwa na meno ya tembo yenye thamani ya Sh bilioni 13.
Katika kesi ya jana, askari huyo, Konstebo mwenye namba za usajili G 5226, ambaye tayari ameshafukuzwa kazi, anaishi katika nyumba za Polisi Ukonga Dar es Salaam na alipanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na mwenzake Hamisi Mwanya maarufu kwa jina la Ussi (22).
Washtakiwa walipofikishwa mahakamani, Wakili wa Serikali, Mwanaisha Komba, aliwasomea mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi, Nyigulila Mwaseba.
Akisoma shtaka hilo, Wakili Mwanaisha alidai kwamba, Julai 19, mwaka huu, eneo la Tazara wilayani Temeke, Dar es Salaam, washtakiwa walikutwa wakimiliki meno ya tembo manne na vipande 12 vya meno hayo, yenye thamani ya Sh milioni 121.5 mali ya Serikali.
Kutokana na uzito wa shtaka hilo, washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo. Pamoja na hayo, Wakili Mwanaisha alidai upelelezi haujakamilika.
Wakati Wakili Mwanaisha akisema hayo, Hakimu Nyigulila alisema shauri hilo haliwezi kusikilizwa mahakamani hapo, badala yake linatakiwa lisikilizwe katika Mahakama Kuu ya Tanzania.
Kutokana na hali hiyo, alisema litakuwa likitajwa mahakamani hapo hadi upelelezi utakapokamilika na kwamba washtakiwa hawatadhaminiwa kwa mujibu wa sheria.
Shtaka liliahirishwa hadi Agosti 7 mwaka huu litakapotajwa tena.
Wakati huo huo, Ofisa Uvuvi wa JKT, Seleman Chasama ambaye anadaiwa kukutwa na meno ya tembo yenye thamani ya Sh bilioni 9, alipanda tena kizimbani hapo wakati shauri lake lilipokuwa likitajwa.
Mshtakiwa huyo anakabiliwa na kesi mbili tofauti za kukutwa na meno ya tembo ya Sh bilioni 9 na nyingine ya kutuhumiwa kukutwa na meno hayo yenye thamani ya Sh bilioni 4.2.
Kesi hizo zipo mbele ya Mahakimu Sundi Fimbo na Nyigulila Mwaseba na zitatajwa tena Agosti 7, mwaka huu.

Chanzo:
Mtanzania
0 comments:
Post a Comment