Home » » News Alert: Mmiliki wa Home shopping Centre, amwagiwa tindikali!

News Alert: Mmiliki wa Home shopping Centre, amwagiwa tindikali!

Katika picha, ni eneo lilipotokea tukio la kumwagiwa Tindikali

Taarifa za awali zinadai kamwagiwa Tindikali maeneo ya Msasani City Mall muda wa saa 2.

Ni jirani na Ubalozi wa Marekani na jirani kabisa na Police Oysterbay.

Jamaa aliyefanya kitendo hicho alitoka mbio, mlinzi akamkimbiza lakini bahati mbaya akateleza na kuanguka na jamaa akawahi pikipiki na kutoweka eneo la tukio.

Said amelazwa Trauma (AMI) Hosp - Masaki.

Kapata madhara macho yote mawili ila moja ndilo limeumia zaidi sehemu ya juu.

Mwenyewe anaweza kuzungumza japo amefungwa mashine sehemu ya pua na madaktari wanamhudumia.

Polisi wanahaha kutafuta wahusika kwa nguvu kubwa na huenda akakamatwa mhusika mapema sana.

 
Chanzo: JF

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa