Home » » WAKILI ERASTO LUGENGE NUSURA AMUUE POLISI KWA RISASI MAENEO YA BOKO.

WAKILI ERASTO LUGENGE NUSURA AMUUE POLISI KWA RISASI MAENEO YA BOKO.




Gari la Wakili Erasto baada ya kugonga 
likiwa Kituo cha Polisi Wazo Hill.
Na Makongoro Oging'
ASKARI polisi wa usalama 
barabarani wa Kituo cha 
Oysterbay jijini Dar es Salaam, 
Amani Leon amenusurika kuuawa
 kwa risasi na Wakili Erasto
 Lugenge wakati akipima ajali ya magari.
Tukio hilo lilitokea Julai 13,
 mwaka huu, saa 6.30 usiku 
Boko CCM, wilayani Kinondoni 
ambapo askari huyo alimtaka 
Lugenge wafike kituoni kutoa maelezo.
Chanzo chetu cha habari 
kimeeleza kwamba Leon alipata
 taarifa kwamba Leon alipata 
taarifa kwamba kuna ajali
 imetokea maeneo ya Boko
 CCM ambapo alienda 
kutekeleza wajibu wake ikiwa
 ni pamoja kupima jinsi ajali ilivyotokea.
“Askari huyo alipofika eneo 
la tukio alikuta gari la Lugenge 
lenye namba za usajili T 181
 DMM aina ya Mark II Grande
 limegonga kwa nyuma gari 
namba T 347 CAR Toyota Rav 4
 lililokuwa likiendeshwa na 
James Mushi ambaye alimtaka
 Lugenge waende kituoni kutoa 
maelezo pia kupimwa kama 
alikuwa amelewa,” kilisema chanzo.
Kiliendea kudai kwamba gari 
la kuvuta magari ‘break down’
 lilifika katika eneo hilo lakini 
Wakili Lugenge ambaye zamani
 alikuwa polisi mwenye cheo
 cha mkaguzi aligoma 
kwenda kituoni.NA GPL


...Gari la wakili kwa nyuma.


Imeelezwa kwamba
 vurumai ikaanza ambapo wote 
walidondoshana chini, Leon 
alimuona Lugenge akichomoa
 bastola kiunoni akitaka
 kumpiga risasi lakini aliwahi 
kumgonga mkono kisha 
bastola ikadondoka chini.
Taarifa zaidi zinaeleza kwamba 
Leon aliiwahi ile silaha na 
kumwamuru Lugenge atii amri 
ambapo alinyosha mikono juu
 ila alikataa kwenda kituoni ndipo
 askari yule aliamuru gari livutwe
 hadi Kituo cha Polisi Wazo Hil
l na ile bastola akaikabidhi kituoni hapo.
Imeelezwa kwamba tayari Lugenge
 anashikiliwa kituoni hapo na
 Leon alikwenda kutibiwa katika
 Hospitali ya Mwananyamala.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa 
Kipolisi Kinondoni, ACP Camilius
 Wambura alipoulizwa juu ya
 sakata hilo alikiri kuwepo.
“Lugenge tunamshikilia kwa
 upelelezi na wakati wowote
 tutamfikisha mahakamani 
tukimaliza uchunguzi wetu. 
Sikutegemea wakili kufanya
 kitendo hicho kibaya,”
 alisema Kamanda Wambura.
CHANZO GLOBAL PUBLISHERS

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa