Na Ali Issa – Maelezo Zanzibar 30/7/2013
Wizara ya kilimo na Maliasili Zanzibar imeiangamiza misumeno 57 ya
moto ili kuepusha ukataji wa miti kwa idadi kubwa na kupelekea
uharibifu wa mazingira Nchini.
Hayo yamesemwa leo huko Baraza lawakilishi na Naibu Waziri wa Wizara
hiyo Amina Iddi Mabruok wakati alipokuwa akitoa Majumuisho ya michango
na maswali ya wakilishi wa wananchi majimboni.
Amsema wametekeleza azma hiyo kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya
ukataji wa miti jambo ambalo lina tishia kukifanya kisiwa kuathiriwa
na mabadiliko mabaya ya tabia ya nchi na kukipotezea uhalisi wake.
“tume ingamiza misumeno hii kuinusuru miti,”alisema Naibu Waziri huyo.
Aidha alisema Rasimu ya kuwea mikakati suala hilo tayari imeandaliwa
kulikomesha suala hilo na wizara ishapiga marufuku kuletwa misomeno
hiyo katika nchi ya Zanzibar.
Nae kaimu wa Wziri wa Wizara hiyo Ramadhani Abdalla Shabani akijibu
hoja za wakilishi mbali mbali juu ya suala la mazao ya Machungwa
kuvamiwa na wadudu huko katika kijiji cha kitogani mkoa wa kusini
Unguja, alisema wizara yake itaongeza mitego ya kuwatega wadudu
waharibifu juu ya zao hilo.
Alisema katika kuhakikisha zao hilo lina fanikiwa alisema atakwenda
yeye na tume yake kuwaonawakulima hao ili kuiona hali hiyo.
Waziri aliwatahadharisha wakulima mara wanapo ona hali mbaya ya
machungwa kuharibiwa na wadudu wayazike ili wadudu wasiendelee kuenea
kuharibu zaidi.
Pia akijibu suala la shamba la Makurunge kupewa chuo cha kizimbani kwa
shughuli za kiutafiti alisema kua tayari wizara imeshaanda hakimiliki
kupewa chuo hicho kuliendeleza eneo hilo kwa shughuli za chuo cha
kizimbani.
Waziri alisema upungufu wakushuka mazao ya chakula kua tani 6000 mwaka
2012 -13 kulitokana na hali mbaya ya hali ya hewa.
Aidha akijibu suala la Serikali kuwa na mpango wa kuweka cha kula cha
hakiba, alisema Wizara yake tayari imeshaanda maelekezo namna ya
kuhifadhi chakula hicho na rasimu ya maelekezo iko serikalini.
“Hifadhi ya chakula inahitaji utaalamu kwani chakula cha kuhifadhiwa
sio mchele , ngano ,sukari vitu hivi vina haribika mapemasana tafauti
na ulivyo ngano,mahindi na vyakula vyote vya maganda.
Mengine waziri huyo akijibu alisema wizara katika kuwapa elimu
wakulima ataongeza na kuwasomesha Mabwana shamba kutoa elimu zaidi kwa
wakulima ilikufanikiwa katika mavuno yao.
0 comments:
Post a Comment