Siku za mwizi ni 40....
Kauli hiyo ya wahenga ilitimia Jumatatu iliyopita kufuatia msichana Pili
Baraka (21) aliyevishwa pete ya uchumba na mpenzi wake hivi karibuni
kujikuta akitupwa Gereza la Segerea jijini Dar baada ya kunaswa kwa
tuhuma za ukahaba,
Mrembo huyo alifikishwa kwenye Mahakama ya Sokoine Drive (Jiji) na
kusomewa shitaka na mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo, Richard Magodi
mbele ya Hakimu Timothy Lyon.
Akisoma shitaka hilo, Magodi alisema: Agosti 5, mwaka huu, saa nane
usiku, Pili alinaswa kwenye maeneo ya Manzese jijini Dar akifanya
biashara ya ukahaba.
Aliposomewa shitaka lake hilo, Pili aliinamisha kichwa na kujibu kwa kifupi: Si kweli.
Licha ya kukana shitaka hilo, Hakimu Lyon alimtaka mchumba huyo wa mtu
kutafuta wadhamini wawili lakini aligonga mwamba na kupelekwa Gereza la
Segerea mpaka Agosti 20, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Akijitetea kabla ya kupandishwa kwenye karandinga kwenda Segerea, Pili
aliiomba mahakama hiyo imuonee huruma asiende kuilia Sikukuu ya Idd,
Segerea kwa kuwa mchumba’ake yuko safarini kikazi na hakuwa na mtu
mwingine wa kumwekea dhamana, ombi ambalo lilikataliwa.
CHANZO GPL
0 comments:
Post a Comment