Bajaji wakiwa kwenye foleni
kuwekewa mafuta na mtu ambaye hakutaka kujitambulisha
*******************
Mwanamme mmoja, ambaye
amekuwa akiongozana na maaskari polisi wawili, amekuwa akigawa fedha za bure
kwa watu mbalimbali jijini Dar.
Kijana huyo wa makamo,
ambaye kwa wiki hii nzima amekuwa akitajwa kwenye radio mbalimbali, aliwalipia
bili wagonjwa wote waliokuwa wamelazwa hospitali ya Mwanyamala na Muhimbili,
wodi ya wanawake.
Alkizungumza na mwandishi
wetu,mmoja wagonjwa wa hospitali ya Muhimbili, Subira Juma alisema kijana huyo
alikuja hospitali na kuuliza wangapi wanadaiwa halafu akawalipia bili zao na
kisha kuondoka zake bila kujitambulisha.
‘Kwa kweli hata mimi
sifahamu kijana huyu katokea wapi, lakini sijwahi kuona mtu akitoa hela bila kujuana,
na kisha kuondoka billa kusema lolote’ alisema Subira.
Wakati huo huo, wasafiri
wa daladala nao, hasa ziendazo Mbagala nao wametajwa kunufaika na mgawo huo,
ambapo wamekuwa wakilipiwa nauli mara kadhaa na mtu huyo.
Mbali na kulipia watu usafiri, kijana huyo pia anatajwa kuwanufaisha maderva boda boda na bajaji kwa kuwawekea mafuta kwenye vyombo vyao vya usafiri.
CHANZO JIACHIE BLOG
0 comments:
Post a Comment