Home » » YANGA YAHAIRISHA MKUTANO MKUU WA DHARULA

YANGA YAHAIRISHA MKUTANO MKUU WA DHARULA

UONGOZI wa Yanga uliitisha mkutano Mkuu wa dharura uliokuwa ufanyike  tarehe 18 Agost 2013 viwanja vya sabasaba kwenye ukumbi wa PTA Saa 3:30 Asubuhi kwa lengo la kujadiliana na suala la Azam Television kurusha mechi za Yanga. 

Mkutano huo kwa sasa umeahirishwa kutokana na sababu  ifuatayo Tarehe 14.8.2014 Naibu Waziri wa Habari, Utamadun,Vijanai  na Michezo Mheshimiwa Amosi Makala aliitisha kikao cha pamoja ,kilichojumuisha pande zote husika wakimwemo  wasaidizi wake, shirik
isho la mpira wa miguu Tanzania(TFF),Mtendaji mkuu wa bodi ya Ligi ya vodacom , uongozi wa Yanga sc na uongozi wa Azam Media.

Baada ya kikao hicho yafuatayo ni makubaliano yaliyofikiwa (a)Klabu ya Yanga itapata fursa ya kushiriki na kupitia katika utengenezaji wa mkataba  wa udhamini wa haki za matangazo na televisheni  wa Azam Media ili kujiridhisha na vipengele vyote vya mikataba kwamba kwa namna yoyote haviathiri klabu ya Yanga kufuatia uhusiano uliopo wa Azam Media wanaotarajiwa kupewa haki hizo na Timu ya Mpira  Azam FC moja ya timu pinzani ya Yanga kwenye ligi ya Vodacom.

(b)Kuwepo na utayari kwa uongozi wa Azam Media kukutana na uongozi wa Yanga kuzungumzia mahusiano ya kibiashara yatakayo nufaisha pande zote mbili.

Hivyo basi baada ya kuzingatia hayo uongozi unapenda kutoa taarifa kwa wanachama wake kuwa mkutano uliopangwa kufanyika tarehe 18 Agosti 2013, viwanja vya sabasaba kwenye ukumbi wa PTA Saa 3:30 asubuhi umeahirishwa hadi mtakapotangaziwa vinginevyo, lengo ni kutoa nafasi na fursa kwa uongozi kufanyia kazi hayo yaliyotajwa hapo juu.

Pia uongozi unawashukuru wanachama na wapenzi wote wa Yanga kwa kuonyesha ukomavu na kusimamia maendeleo  ya klabu yetu kwa Hali na mali, na uongozi Utaendelea kusimama IMARA katika kuijenga Yanga Mpya
Uongozi pia unawataka wapenzi wote kuja kwa wingi uwanjani kuishangilia timu yetu wakati wa mechi ya kugombea ngao ya hisani kuashiria ufunguzi wa michuano ya kutetea ubingwa tunaoushikiria  wa Ligi Kuu ya vodacom.

Clement Sanga
Makamu Mwenyekiti
Young Africans Sports Club
16.08.2013

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa