Mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Afrika Mashariki,
Mhe. Adam Kimbisa akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Katibu wa wabunge wa
Tanzania katika bunge hilo, Shy-Rose Bhanji, mbunge wa bunge hilo,
Nderakindo Kessy na kulia ni Mhe. Makongoro Nyerere.
Katibu wa wabunge wa Afrika Mashari kutoka Tanzania, Shy-Rose Bhanji
akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Mhe. Nderakindo Kessy na Mwenyekiti wa wabunge wa
Tanzania katika Bunge hilo, Mhe. Adam Kimbisa.
Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania wakibadilisha
mawazo baada ya mkutano wao na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
jana. Kutoka kushoto ni Katibu wa Wabunge wa Afrika Mashariki kutoka
Tanzania, Shy-Rose Bhanji, Mwenyekiti, Adam Kimbisa, Nderakindo Kessy na
Makongoro Nyerere.
Mbunge la Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania Mh. Makongoro
Nyerere akipeana mkono na Katibu wa wabunge wa Tanzania katika Bunge
hilo, Mhe. Shy-Rose Bhanji.
DAR ES SALAAM, Tanzania
Bunge la tatu EALA limeridhia Tanzania kupata kikao chake rasmi ambapo
sasa kikao kitafanyika Dodoma na vikao vingine viwili kufanyika Arusha
ambayo ni Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania, mhe. Adam Kimbisa amesema hayo katika
mkutano na wabunge watanzania EALA, na waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam, leo.
Mhe. Kimbisa amesema katika ratiba ya vikao vya Bunge la EALA, Tanzania
pia imepata rasmi kikao kimoja ambapo sasa kitafanyika mjini Dodoma.
Vile vile amesema kikao hicho kinaweza kufanyika Dar es Salaama au Zanzibar.
Amefafanua kwamba, Bunge limeridhia vikao viwili vifanyike Arusha,
kimoja kifanyike Tanzania sambamba na nchi zingine wanachama; Kenya,
Uganda, Rwanda na Burundi kupata kikao kimoja kila nchi kwa mzunguko.
Amesema nchi ambayo itakosa kikao kwa mwaka huu wa fedha 2013/2014, ndio
itakuwa nchi ya kwanza kupata kikao cha mwaka ujao wa fedha.
Hata hivyo amesema, vikao vikao viwili vya Arusha vitakuwa ni vikao vya
bajeti na ukaguzi wa mahesabu ambavyo ni vikao muhimu sana katika Bunge.
Mhe. Kimbisa amesema kikubwa wananchi wanachotakiwa kufahamu ni kuwa
linapokuja suala la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Arusha ni Makao Makuu
na kwamba haiko Tanzania kwani nchi zote tano ni wadau wa Arusha.
Naye Katibu wa watanzania, Shy-Rose Bhanji amesema ni jambo la kujivunia
kwamba Tanzania sasa itakuwa na kikao rasmi kwa njia ya mazungumzo. Hii
ni hatua nzuri vile wananchi pia watapata mwamko wa masuala
yanayojadiliwa Bungeni.
Hatua ya maridhiano hayo imefuatia mgoghoro ulioibuka miongoni mwa
wabunge wa EALA kwamba vikao vya Bunge hilo vifanyike Arusha kwa mwaka
mmoja wa fedha na si kwa mzunguko kama ilivyozoeleka kuanzia Bunge la
pili.
Wabunge wengi isipokuwa watanzania walitaka vikao viendelee kwa mzunguko nchini Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Arusha.
Vikao vya EALA hadi mwaka wa fedha June 2012/June 2013 vilikuwa vitano
kwa mwaka. Vikao hivyo vimeongezeka kuwa sita. Vikao hufanyika kila
baada ya takriban miezi miwili, kwa kipindi cha wiki mbili.
CHANZO: VIJIMAMBO BLOG
0 comments:
Post a Comment