Mshindi
wa taji la Taifa la Miss Utalii Tanzania 2012/2013, Hadija Saidi Juma
Mswaga, ambaye pia ni Miss Utalii Morogoro 2012/13, ataondoka nchini
28-9-2013 kwenda nchini Equatorial Guinea, ambako Fainali za Dunia za
Miss Tourism World 2013/14 zinafanyika Tarehe 12-10-2013 katika ukumbi
wa kimataifa wa Sipopo Conference Centre Malabo Equatorial Guinea.
Kwa
mujibu wa Taarifa iliyo tolewa na Fredy Njeje, mkurugenzi wa Habari na
Masoko wa Miss Tourism Tanzania Organisation (MTTO), jumla ya washiriki
kutoka nchi 126 Duniani watashiriki katika mashindano hayo ya
Dunia,ambayo mwaka Jana yalifanyika nchini Thailand ambapo mrembo Tatyana Maksimova kutoka nchini Urusi alishinda Taji la Miss Tourism World 2012/13.'
Hii
itakuwa ni mara ya nne kwa Tanzania kushiriki mashindano hayo ya Miss
Utalii Dunia, ambapo kila mwaka kuanzia mwaka 2005 tumeshinda mataji,
Mataji hayo na washindi kutoka Tanzania katika mabano ni Miss Tuourism
World 2005- Africa (Witness Manwingi – Tanzania), Miss Tourism World
2006 – SADC (Killy Janga – Tanzania), Miss Tourism World 2007 – Africa
(Lillian Cyprian – Tanzania), Miss Tourism World 2008- Internet ( Lilly
Kavishe – Tanzania) na Miss Tourism Model Of The World 2006 –Personality
( Witness Manwingi – Tanzania). '
Tangu
mwaka 2008, Tanzania haikushiriki katika mashindano hayo kutokana na
kutokana na kukosa wadhamini wa safari hizo na matatizo mengine ya
kiufundi yaliyo pelekea mashindano hayo kutofanyika nchini tangu 2008-
2010. Njeje alisema kuwa, Miss Utalii Tanzania 2012/2013, Hajija Saidi
Juma Msugwa, anajukumu zito zaidi ya washiriki wengine wote walio
tangulia kwani anakazi ya kwenda kulinda heshima ya Tanzania na
kudumisha rekodi ya Miss Utalii Tanzania ya kutokushindwa katika
mashindano yoyote ya kimataifa na Dunia.
Nae
Miss Utalii Tanzania 2012/13, Hajija Saidi Juma Mswaga, amesema kuwa
anatambua jukumu kubwa na zito alilonalo la sio kutangaza Utalii na
Utamaduni wa Tanzania tu, bali kulinda heshima ya Tanzania na Mashindano
ya Miss Utalii Tanzania ya kutowahi kushindwa katika mashindano yoyote
ya kimataifa.
“Nawaomba
watanzania waniombee na kunipa ushirikiano wa hali na mali katika
kufanikisha maandalizi yangu na safari ya kupeperusha bendera ya Taifa
katika medani ya kimataifa”. Shindano la Miss Tourism World 2013,
litarushwa na kuonyeshwa LIVE katika nchi zaidi 130 Duniani kote na
kushudiwa na zaidi ya watazamaji 650 Milioni Duniani kote, huku
washiriki wakipewa fulsa ya kuonyesha vivutio vya utalii vya nchi zao,
kupitia vyombo mbalimbali vya habari vya Televisheni, Majarida na
Mitandao.
Regards
Erasto Gideon Chipungahelo
President Miss Tourism Tanzania International - The Symbol Of National Heritage
0 comments:
Post a Comment