Mwanamuziki
kutoka Ghana, Fuse ODG, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
burudani yake kesho kwenye uwanja wa Ustawi wa Jamii. Pembeni yake ni
Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan.
Fuse
ODG akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari, kulia kwake ni Afsa
Biashara wa Zantel, Sajid Khan, akifuatiwa na Hermes wa BHitz, na mwanzo
kushoto ni Mkurugenzi wa Times FM, Rehure Nyaulawa.
Fuse ODG akicheza Azonto na baadhi ya mashabiki.
************************
Kutoa burudani kali viwanja vya Posta kesho
Mwanamuziki
mashuhuri kutoka nchini Ghana, Fuse ODG, kesho anatarajiwa kutoa
burudani kali kwenye viwanja vya Ustawi wa Jamii hapa jijini Dar es
Salaam.
Mwanamuziki
huyo ambaye anatamba na wimbo wake wa Azonto, analetwa kwa ushirikiano
wa kampuni ya simu za mikononi ya Zantel, pamoja na Times FM.
Burudani
hiyo inatarajiwa itaanza kuanzia mida ya saa mbili usiku hadi majogoo
kwa kiingilio cha shilingi elfu kumi kwa kununua tiketi kabla na elfu
kumi na tano kwa watakao nunua tiketi mlangoni.
Akimzunguzia
mkali huyo, Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan, alisema Zantel
imemleta msanii huyo ili kuwapa ari wasanii wa ndani wenye lengo la
kufikisha kazi zao hatua za kimataifa.
‘Zantel
imekuwa msitari wa mbele katika kuwawezesha wasanii wa ndani, hasa
vijana, na kwa kumleta Fuse ODG, ambaye ni mmoja wa wasanii wachache
kutoka Afrika waliofanikiwa kufikisha mziki wao soko la kimataifa
tunaamini vijana watajifunza mengi’ alisema Khan.
Fuse
ODG ni mwanamuziki wa Ghana mwenye makazi nchini Uingereza, ambaye
wimbo wake wa Azonto ulifanikiwa kuwa namba moja kwenye iTunes World
Chart, akiwa ni mwanamuziki wa kwanza kutoka Ghana kufikia mafanikio
hayo.
Kwa wimbo wa Azonto pekee, Fuse ODG alifanikiwa kupata watazamaji zaidi ya milioni kumi na moja kwenye You Tube kwa mwaka 2012.
Naye
Mkurugenzi wa Times FM, Rehure Nyaulawa, alisema wamemleta msanii huyo
ili kuhakikisha watanzania wanapata burudani wanayoipenda ya Azonto hapa
hapa nchini.
‘Azonto
imejipatia umaarufu mkubwa karibu dunia nzima, lakini pia kwa upande wa
radio yetu wimbo huu umepata maombi mengi kuliko wimbo wowote wa
kimataifa kiasi cha kuona tuwaletee watanzania burudani wanayoipenda’
alisema Nyaulawa.
Fuse
ODG atasindikizwa na wasanii wote wa kundi la BHitz, Mshindi wa Epiq
BSS Walter Chillambo, Menina pamoja na wasanii wa Marco Chali
Foundation.
Wimbo wake mpya wa Antena ambao amemshirkisha Wyclef Jean unafanya vizuri kwenye chati mbalimbali duniani kwa sasa.
0 comments:
Post a Comment