RAIA wawili ndugu wa Kenya, Mark Rubila (16) na
Sila Rubila (21) wanaodaiwa kumuua dereva teksi, Ramadhani Mahembe (38) mkazi
wa Buguruni Chama, wameanza kufichua siri mbalimbali kuhusu matukio mbalimbali
ya ujambazi ambayo wamekuwa wakiyafanya.
Kwa mujibu wa chanzo chetu ndani ya Jeshi la
Polisi, Wakenya hao kutoka mji wa Kakamega wameshafanya matukio mengi ya
ujambazi yakiwamo ya uporaji magari.
“Wahenga wanasema siku za mwizi ni arobaini, hivyo
ndivyo inavyodhihirika kwa Wakenya hao ambao wamefichua siri zaidi kuhusu
ujambazi waliokuwa wakiufanya na kueleza kuwa gari walilotaka kumpora marehemu
Mahembe walitaka kulipeleka mkoani Tanga kwa mteja.
“Hao vijana ni wadogo kiumri lakini wanaonesha ni
hatari sana kwani wameeleza kuwa wameshafanya matukio mengi yakiwamo ya kuiba
magari mengi, walipoulizwa ilipo Toyota Hilux walisema walilificha sehemu
mkoani Tanga,” kilieleza chanzo kingine.
Baada ya kubanwa zaidi inadaiwa kuwa watuhumiwa hao
waliwaeleza polisi kuwa awali walimpelekea mteja gari aina ya Toyota Hilux na
alilikataa na kuwaeleza kuwa anataka gari dogo.
Chanzo hicho kinadai kuwa watuhumiwa hao walitaja
watu kadhaa ambao wamekuwa wakishirikiana nao.
Siku za hivi karibuni matukio ya ujambazi yamekuwa
yakiliandama Jiji la Dar es Salaam mfululizo kwa benki za watu binafsi kuporwa
mamilioni ya fedha.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment