Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » BEN KINYAIYA AIBIWA VITU KWENYE GARI YAKE

BEN KINYAIYA AIBIWA VITU KWENYE GARI YAKE


MTANGAZAJI wa Kipindi cha Mama Land, kinachorushwa na Runinga ya Clouds ya jijini Dar, Benny Kinyaiya hivi karibuni alikombwa vitu kadhaa kwenye gari lake na vibaka mara baada ya kupaki gari nje ya nyumba yake.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Kinyaiya alisema kuwa siku ya tukio saa nne usiku aliporejea nyumbani kwake maeneo ya Kinondoni Dar, aliegesha gari nje ya geti na kuingia ndani kuchukua kitu kisha aendelee na mishemishe zake.
Habari zinapasha kwamba, baada ya kuingia wezi hao walitumia fursa hiyo kuvunja vioo na kuiba redio na vitu vingine.
“Inauma sana kwani kilikuwa ni kitendo kama cha dakika chache tu, yaani kuingia ndani na kutoka tu tayari nimeshaibiwa, natamani hata nimkamate mmoja ili nimuoneshe mfano,” alisema Kinyaiya.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa