Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akisalimiana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Diana Melrose (kulia) leo katika viwanja vya michezo vya shule ya sekondari Kibasila wakati wa Bonanza la mchezo wa mpira wa miguu lililohusisha vijana kutoka katika vituo 19 vya kulelea watoto walio katika mazingira magumu vya jijini Dar es salaam.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Diana Melrose (kushoto) akipiga mpira kuashiria kuanza kwa Bonanza la mchezo wa mpira wa miguu lililohusisha vijana kutoka katika vituo 19 vya kulelea watoto walio katika mazingira magumu vya jijini Dar es salaam. Kulia anayeonekana kudaka mpira huo ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Diana Melrose (kulia) akikagua timu ya mpira ya FC Kigamboni kutoka kituo cha kulelea watoto walio katika mazingira magumu cha Kigamboni kabla ya kuanza kwa michuano ya kuwania kombe katika bonanza lililovihusisha vituo 19 vya kulelea watoto walio katika mazingira magumu vya jijini Dar es salaam.
Mashindano hayo yaliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Ubalozi wa Uingereza,British Council, Baraza la Michezo Tanzania, na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo yakiendelea katika viwanja vya michezo vya shule ya sekondari Kibasila leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa British Council nchini Tanzania Bw.Richard Sunderland akikagua timu ya mpira ya kituo cha kulelea watoto walio katika mazingira magumu cha Dogodogo leo katika viwanja vya michezo vya shule ya sekondari Kibasila.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (kulia) akimvisha medani kijana Juma Abdul wa kituo cha kulelea watoto walio katika mazingira magumu cha Kigamboni leo jijini Dar es salaam.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Diana Melrose (kushoto) akizungumza jambo na Arafa Abdul Kutoka kituo cha mpira wa miguu cha Twalipo (Twalipo Camp Soccer Foundation) leo jijini Dar es salaam. Arafa Abdul alikua mmoja wa waamuzi wa Bonanza la mchezo wa mpira wa miguu lililohusisha vijana kutoka katika vituo 19 vya kulelea watoto walio katika mazingira magumu vya jijini Dar es salaam.
Washindi wa jumla wa Bonanza hilo timu kutoka kituo cha kulelea watoto walio katika mazingira magumu cha Dogodogo wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi kutoka Wizara ya Habari, Ubalozi wa Uingereza, Baraza la Michezo Tanzania,Right to Play Tanzania mara baada ya kunyakua kombe na medali mbalimbali.
.Washindi wa jumla wa Bonanza hilo timu ya mpira wa miguu kutoka kituo cha kulelea watoto walio katika mazingira magumu cha Dogodogo wakifurahia ushindi mara baada ya kutangazwa leo jijini Dar es salaam.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Diana Melrose (kulia) akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo mara baada ya kukamilika kwa Bonanza la mchezo wa mpira wa miguu lililohusisha vijana kutoka katika vituo 19 vya kulelea watoto walio katika mazingira magumu vya jijini Dar es salaam.Kushoto ni Mkurugenzi wa British Council nchini Tanzania Bw. Richard Sunderland.
Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.
Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.










0 comments:
Post a Comment