Na. Mwandishi wetu
HOTELI
ya Double Tree by Hilton ya jijini Dar es Salaam yatoa msaada wa
mashuka, mataulo kwa kituo cha Kulelea Watoto yatima cha SOS Children
Villages katika muendelezo wao wa kusaidia jamii na watoto waishio
katika mazingira magumu.
Akizungumza
na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dar, Mkurugenzi wa Mauzo wa
Hoteli ya Double Tree by Hilton, Bw, Florenso Kirambata amesema
wameamua kugawa msaada huo kwa sababu wao ni sehemu ya jamii.
“Tumeamua
kugawa msaada huu kwa kuguswa na matatizo mbalimbali wanayokabiliana
nao vituo vingi vya kulelea watoto hapa nchini katika harakati zetu za
kuhahikisha watoto yatima wanapata mahitaji muhimu katika maisha yao ya
kila siku,” amesema.
Amesema
baadhi ya msaada uliotolewa ambao ni jumla ya piece 984 yakiwemo
Mashuka, Duvet Cover (mazulia), mataulo ya kuogea, mataulo ya
kusafishia, mataulo ya kujifutia mkono, Mataulo ya kuogea, Napkins na
Foronya.
Mkurugenzi
huyo Bw, Kirambata amesema Hoteli ya Double Tree imekuwa ikitoa msaada
wa aina hiyo kila baada ya miaka miwili na mwaka uliopita zali
liliwaangukia Hospitali ya Taifa Muhimbili na safari wameona watoe
msaada huo kwa kituo cha SOS Children’s Villages nchini.
Historia
fupi ya Kazi ya Vijiji SOS Watoto katika Tanzania ilianza mwaka 1984.
Kipindi hicho aliyekuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar , Alhaji
Ali Hassan Mwinyi, alikaribisha ombi toka kwa taasisi ya Kijerumani ya
Hermann Gmeiner la kujengwa kituo cha kulelea watoto.
Makubaliano
ya serikali na mfadhili yalisainiwa tarehe 25 Februari 1987. Kijiji cha
SOS Children kilijengwa kati ya 1988 na 1990 na familia ya kwanza
walikuwa na uwezo wa kuhamia katika nyumba za familia kati kati ya 1991.
Kwa
sababu ya uhuru wa kisiasa , SOS watoto Vijiji pia iliamua kufanya kazi
bara na visiwani SOS Children Vijiji Zanzibar na SOS Vijiji ya Watoto
Tanzania bara na walianza rasmi mwezi Aprili 1997. Kijiji kwanza SOS
Watoto Tanzania Bara kilijengwa mjini Arusha, kaskazini mwa nchi.
0 comments:
Post a Comment