WAKALA wa Vipimo nchini (WMA)
anakabiliwa na changamoto mbalimbali katika ukaguzi wa maduka ya nyama (bucha)
zikiwamo za wamiliki kutumia mawe yenye uzito pungufu.
Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana na
Meneja Mkaguzi wa WMA, Richard Kadege, alipozungumza na waandishi wa habari na
kuzitaja changamoto nyingine kuwa ni kutumia mizani isiyotumika kisheria,
kutumia mihuri isiyo na muhuri wa serikali, pamoja na mawe.
Alisema changamoto nyingine ni kuharibu mizani kwa
makusudi ili kuwaibia wateja, mfano kutegua pini za mizani, kuwakimbia
wakaguzi, kunatisha nyama katika sahani pamoja na kuweka smaku katika mizani.
Meneja huyo pia alisema kufunga uzi kwenye binu
upande wa mteja kuelekea chini ya meza na kuwatolea lugha ya matusi na vitisho
vya kisu wakaguzi ni changamoto nyingine.
Pamoja na changamoto hizo, Kadege alisema Wakala
aliitisha kikao cha wadau wa maduka ya nyama jijini ambapo uamuzi ulikuwa ni
kuitisha kikao cha pamoja kati ya wauza nyama, wamiliki na Wizara ya Kazi na
Ajira.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment