Mkurugenzi wa UHAI Tanzania Deus
Nshekanabo (kushoto) na Aliyejitambulisha kama Katibu wa umoja wa
waendesha bajaji, bodaboda Wilaya ya Kinondoni Uwesu Mohamed.
Waendesha
bodaboda, bajaj mkoa wa Dar es Salaam wagoma kuhudhuria mkutano ulioandaliwa na
Asasi ya Uhai Tanzania wakidai kuwa harufu ya ulaghai na ufisadi inanukia
katika asasi hiyo.
Wakiongea na
mtandao huu wamesema hawana imani na Mkurugenzi wa UHAI Tanzania Deus Nshekanabo ambaye ndiye
ameandaa mkutano huo kwa waendesha bodaboda na bajaji mkoa wa Dar es Salaam ili
kuwapa elimu na maarifa yakuanzisha Benki ya Vijana iitwayo Ajira Vijana
Foundation Bank –AVFB uliokuwa umeandaliwa na asasi ya kitaifa ya afya ya umma
(UHAI Tanzania) United Health Action Initiatives-UHAI.
Makamu Mwenyekiti, Rangi
Makamu
Mwenyekiti wa Umoja wa Bodaboda na bajaj Afrika Sana, Musdicky Rangi amesema
wanachama wake wameshindwa kuhudhuria mkutano huo baada ya kupata taarifa kuwa
asasi hiyo imekuwa ikitapeli vijana.
“Vijana
wamekataa kuja kwenye mkutano huu kwa kuwa kuna mambo mengi hayajawekwa wazi,
hatujui Uhai ni kitu gani, wamesajiliwa ama la, halafu anakuja hapa na gia ya
kutumia majina ya marais wastaafu wakidhani tutawaanmini kirahisi” anasema
Rangi na kuongeza kuwa:
“Kama kweli
anahitaji kufanya mkutano wa kuanzisha benki ya vijana, kwanini wanatuletea
watu ambao hata hawaeleweki, tumemuuliza maswali amebaki akijiumauma tu, kuna
dalili ya ufisadi na utapeli hapa”
Awali Asasi
hiyo iliandaa mkutano huo ambao ulipangwa kufanyika leo Octoba 14 kwenye ukumbi
wa HEKO HALL Sinza Afrika Sana kuanzia saa
tatu kamili aubuhi uligonga mwamba baada ya waandaaji kuhusishwa na utapeli.
Pamoja na
kutangaza kuwa lengo la mkutano huo kukutana na madereva wa bajaji na bodaboda
ili kujadili mambo ya uanzishaji benki ya vijana ni kuwakuza nakuwatoa sekta
isiyo rasmi kwenda sekta iliyo rasmi ya biashara mkutano huo uligubikwa na
ubabaishaji mwingi.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Uhai Tanzania Deus Nshekanabo anasema mkutano wa leo
ulipanga kuwapata vijana watakaoshiriki kwenye mkutano wa uvumbuzi wa mafanikio
ya marais wastaafu uliopangwa kufanyika Octoba 25 mwaka huu kwenye hoteli ya
Serana.
Hotuba ya Rais Kikwete
Lakini jambo
kubwa lililowashtua madereva bajaji wachache waliofika kweny ukumbi wa Heko ni
ile nakala ya hatuba ya mkutano huo wa tarehe 25 ambayo inaonyesha kuwa mgeni
rasmi katika mkutano huo atakuwa ni Rais Jakaya Kikwete, akiambatana na marais
wastaafu wote, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, wakuu wote wa mikoa
0 comments:
Post a Comment