Home » » ‘Wataalamu kujenga ghorofa kwa siku’

‘Wataalamu kujenga ghorofa kwa siku’



na Mwandishi wetu

WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, amesema kuanzia sasa watapunguza tatizo la ukosefu wa nyumba kwa watumishi wa serikali baada ya wataalamu kupata utaalamu wa kujenga ghorofa moja kwa siku.
Mbali na hilo, Wakala wa Majengo nchini (TBA) umepanga kununua vifaa vya kupima ubora wa majengo ya serikali wakati na baada ya utekelezaji wa ujenzi kukamilika.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa nyumba 851 zinazojengwa na TBA katika eneo la Bunju ‘B’, Kinondoni, Dk. Magufuli alisema jambo hilo litaonekana ni la kushangaza, lakini linawezekana kutokana na kuwepo kwa teknolojia ya kisasa.
Dk. Magufuli alisema serikali ilipeleka wataalamu nchi mbalimbali kujifunza teknolojia hiyo, ikiwamo Uturuki ambapo taaluma hiyo itasaidia kupunguza tatizo la makazi kwa watumishi wa umma.
Alisema hadi sasa kuna upungufu wa nyumba milioni tatu nchini na wakala huo umeshapokea maombi mapya 3,000 ya watumishi wa umma wanaohitaji makazi.
Waziri huyo alisema ujenzi wa nyumba hizo ulianza Aprili mwaka huu na ulitumia kikosi cha wakala huo kinachoitwa ‘force Account’ ambacho hadi sasa kimejenga nyumba 155 ambazo zimegharimu sh bilioni 3.9.
Alisema wakala huo unatarajia kujenga nyumba 10,000 nchini kwa kipindi cha miaka mitano ambapo kwa mwaka huu utajenga nyumba 2,500.
Mtendaji Mkuu wa TBA, Asangalwisye Mwakalinga, alisema kununuliwa kwa vifaa hivyo kutasaidia serikali kufahamu majengo yaliyojengwa chini ya viwango na yale ya zamani ambayo hayana ubora ili kuzuia uwezekano wa kutokea maafa.
Aidha, Makamu wa Rais, Dk, Mohammed Gharib Bilal, alisema kuwa mji huo utakapokamilika utajulikana kama Satelite New City ambao utakuwa mfano kwa miji iliyopo pembezoni
CHANZO : DAIMA

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa