Home » » Dawasco yaagiza nyumba Mwenge zivunjwe haraka

Dawasco yaagiza nyumba Mwenge zivunjwe haraka

Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasco)
 
Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasco), imeutaka uongozi wa Chama cha Ushirika wa Ujenzi wa Nyumba Mwenge kubomoa mara moja nyumba zilizojengwa juu ya miundombinu ya majitaka ya mamlaka hiyo.
Aidha, Mamlaka hiyo imemwamuru mwananchi anayejenga kwenye eneo la kiwanja kitalu namba 43 alichouziwa na Ushirika huo kinyume na sheria, kuacha kuendelea na ujenzi huo mara moja vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Ofisa Uhusiano wa  mamlaka hiyo, Eva Lialo, alisema ni makosa makubwa kuzalisha viwanja ndani ya hifadhi ya mabomba makubwa ya Dawasco, yakiwamo ya majitaka kwani yapo kisheria.

Alisema kama hawatavunja nyumba hizo, Dawasco italazimika kuzivunja ili mabomba hayo yaendelee kuwapo katika hali ya usalama.
Akizungumzia tukio hilo, Paul Mrema, mkazi wa eneo hilo kwa miaka mingi alisema wanashangazwa na jinsi uongozi wa Ushirika huo unavyovunja taratibu na kuamua kuuza viwanja kiholela wakati wakijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Mrema alidai kuwa eneo hilo la kitalu namba 43, lilikuwa na viwanja vitano ambavyo vyote vipo juu ya mabomba hayo na linamilikiwa na Dawasco lakini viliuzwa na uongozi wa ushirika huo kwa watu mbalimbali.
 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa