Home » » KINONDONI SASA KUANZA KUNYWA MAJI SAFI NA SALAMA

KINONDONI SASA KUANZA KUNYWA MAJI SAFI NA SALAMA


Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (wa pili kushoto) akiongozwa na viongozi wa Kata ya Manzese kuelekea kwenye ukaguzi wa maendeleo ya Mradi wa Maji Safi na Salama ya Kisima katika Mtaa wa Mivuleni, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Wakazi wa Mtaa wa Mivuleni, Kata ya Manzese, Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam wakichota maji ya mradi wa maji safi na salama ya kisima wa Manispaa hiyo, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuf Mwenda (mbele kulia) akikagua kivuko kinachounganisha Kata ya Sinza na Kijitonyama, Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa Mendeleo ya Ujenzi wa Mradi wa Maji safi na salama ya kisima katika Mtaa wa Sinza E mwishoni mwa wiki.
Mkandarasi wa Kampuni ya Drilling and Dam Construction Agency, Elzei Makaso (kulia) akimelezea Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (kushoto) maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Maji safi na Salama ya Kisima katika Mtaa wa Magomeni Dosi, Dar es Salaam wakati Meya huyo alipofanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo mwishoni mwa wiki.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (kushoto) akizindua Mradi wa Maji safi na salama ya kisima katika Mtaa wa Sinza E, Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo mwishoni mwa wiki. Kushoto kwake ni Diwani wa Kata hiyo (CHADEMA), Renatus Pamba.
Mhandisi wa Maji wa Manispaa ya Kinondoni, Gonzalves Rutakyamirwa (kushoto) akimwelezea Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (mwenye shati ya drafti) maendeleo ya mradi wa Maji safi na salama ya kisima unaotekelezwa kwenye Mtaa wa Mivuleni, Manzese, Dar es Salaam juzi wakati Meya huyo alipofanya ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo kwenye Kata tisa za Manispaa hiyo mwishoni mwa wiki. Kulia kwake ni Diwani wa Kata hiyo, Eliam Manumbu na Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Mipangomiji na Mazingira, Richard Chengula. 
kwa hisani ya michuzi blog

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa