Na Ally Kondo, Kuwait
Serikali
ya kuwait imetenga kiasi cha Dola za Marekani bilioni moja (1) kwa
ajili ya kuzipatia nchi za Afrika mikopo ya masharti nafuu katika
kipindi cha miaka mitano ijayo. Tangazo hilo lililotolewa na Amir wa
Kuwait ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mkutano wa Tatu wa Wakuu wa Nchi na
Serikali wa Ushirikiano baina ya Nchi za Afrika na Kiarabu (Third Afro
Arab Summit), Sheikh Sabah Al-Ahnad Al-Sabah wakati alipokuwa anatoa
hotuba ya ufunguzi ya mkutano huo nchini Kuwait siku ya Jumanne tarehe
19 Novemba, 2013.
Sanjari na kiasi hicho cha fedha, Sheikh Al-Sabah alitangaza kiasi kingine cha Dola za Marekani milioni moja (1) kwa ajili ya kufadhili shughuli mbalimbali za utafiti zenye lengo la kuibua fursa za maendeleo katika nchi za Afrika.
Chanzo;Michuzi blog