Home »
» PONDA ATINGA MAHAKAMA KUU
PONDA ATINGA MAHAKAMA KUU
Mahakama Kuu, Kanda ya
Dar es Salaam, inatarajia kufanyia mapitio ya uamuzi wa kutupilia mbali
ombi la upande wa utetezi la kutaka kufutwa kwa shtaka la kutotii amri
halali ya mahakama linalomkabili Shekhe Ponda Issa Ponda.
Ombi hilo
lilitupiliwa mbali na Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro,
Richard Kabate. Mapitio hayo yanatarajiwa kufanyika Novemba 18, mwaka
huu.
Mawakili wa Ponda wakiongozwa na Juma Nassoro, waliiomba
mahakama hiyo kupitia uamuzi huo uliotolewa Oktoba mosi, mwaka huu na
hakimu huyo.
Hakimu Kibate alitupilia mbali ombi la upande wa
utetezi uliokuwa ukiomba mahakama hiyo kuondoa shtaka hilo la kutotii
amri halali linalomkabili mteja wake au lifutwe akidai kuwa ilitolewa na
Mahakama ya Kisutu.
Wakili Nassoro alidai kwamba amewasilisha ombi
hilo baada ya kubaini kuwa mahakama hiyo ya Morogoro haina uwezo
kisheria kusikiliza shtaka hilo, vinginevyo lifunguliwe katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu ambayo ilitoa hukumu hiyo.
Hatahivyo, Hakimu
Kibate alitupilia mbali ombi hilo na kusema kuwa kwa mujibu wa vifungu
mbalimbali vya sheria vya uendeshaji wa kesi za jinai, shtaka hilo dhidi
ya Ponda la kudaiwa kutokutii amri halali ya mahakama litaendelea
kusikilizwa katika mahakama hiyo na sio kuhamishiwa Kisutu.
Alizitaja
sababu za shtaka hilo kuendelea kusikilizwa katika mahakama hiyo kuwa
ni mshtakiwa huyo kutenda kosa hilo eneo la Kiwanja cha Ndege la
Manispaa ya Morogoro.
Hakimu huyo alisisitiza kuwa hakuna sababu ya kuhamishiwa shtaka hilo katika Mahakama ya Kisutu.
Sababu
nyingine ni mshtakiwa huyo kuvunja amri halali iliyotolewa na Mahakama
ya Kisutu na sio sharti kama ambavyo upande wa utetezi ulidai na
kufafanua kuwa hata kama mahakama hiyo ilitoa sharti, kisheria sharti
linalotolewa na mahakama yoyote ni amri.
Sheekhe Ponda anakabiliwa
na mashtaka matatu anayodaiwa kuyatenda kwenye mhadhara huo. Ilidaiwa
mahakamani kwamba aliwaambia Waislamu wasikubali uundwaji wa kamati za
ulinzi na usalama za misikiti kwani zimeundwa na ambao ni vibaraka wa
CCM na serikali
Chanzo;Majira
0 comments:
Post a Comment