Madaktari na wataaamu wengi wa mambo ya afya na saikolojia wanashauri michezo kutumika kwa wafanyakazi ikiwa ni njia mojawapo ya kuongeza ufanisi wa utendaji kazi, na kuboresha mahusiano katika shirika, taasisi ama kampuni husika
Kwa kuitambua dhana hiyo mfuko wa pesheni PSPF umekuwa mbele kushiriki katika mabonanza mbalimbali ya michezo kwa lengo la kujenga afya na kubadilishana mawazo na watu mbalimbali ndani na nje ya mfuko huo.
Jumapili ya Novemba 17 timu ya mpira wa miguu ya PSPF imeshuka dimbani kumenyana na mahasimu wao Coca Cola katika mtanange ambao uikuwa na upinzani wa hali ya juu na kuufanya mchezo huo kuwa burudani kwa mashabiki waliohudhuria uwanjani hapo.
Shuhudia picha za matukio mbalimbali kutoka kwenye bonanza hilo ambao limefanyika kwenye viwanja vya Tanganyika Packers Kawe.
Msemaji wa timu ya PSPF, Gwamaka Andrew akionyesha jezi ya kipa wa timu yake
Benchi la ufundi
Samweli Haule, Mhasibu wa timu ya PSPF katika picha na shabiki wa timu hiyo
Gwamaka katika picha na wachezaji wa timu ya Cocacola
0 comments:
Post a Comment