JANA uongozi wa klabu ya Simba ulitangaza kumsimamisha mwenyekiti wake Ismail Aden Rage.
Maamuzi hayo yalitokana na kikao cha kamati ya utendaji
kilichofanyika hapo juzi, hizi ni Miongoni mwa sababu zilizotolewa kwenye mkutano wa
waandishi wa habari zilizopelekea kusimamishwa kwa Mheshimiwa Rage.
Rage alisaini mkataba na Azam TV kwa ajili ya kipindi ya cha
Simba TV bila kuishirikisha kamati ya utendaji.
Wakati Rage anasaini mkataba na Azam TV tayari klabu ya
Simba ilikuwa kwenye mazungumzo ya mwisho mwisho kuingia mkataba na kampuni ya
ZUKU kwa ajili kipindi cha Simba TV uliokuwa na thamani ya dola za kimarekani
300,000 kwa mwaka.
Kampuni ya ZUKU ilipokuwa kwenye majadiliano na viongozi wa vilabu
vya Simba na Yanga jijini Nairobi, kwenye mkutano huo Simba iliwakilishwa na Mjumbe wa kamati ya
utendaji Joseph Itang’are maarufu kama mzee Kinesi pamoja na mwanachama Evans
Aveva wakati Yanga iliwakilishwa na Makamu mwenyekiti Clement Sanga na Francis
Kifukwe, viongozi hao Simba Ghafla walisikia Rage kasaini mkataba na Azam TV kwa ajili ya Simba TV.
Mheshimiwa Rage ndiye aliyesimamia uhamisho wa mchezaji Okwi
on CREDIT bila kuishirikisha kamati ya utendaji,matokeo yake klabu hiyo mpaka
leo imeshindwa kupata pesa ya uhamisho wa mchezaji huyo.
Sababu nyingine iliyoelezwa ni kitendo chake cha kushindwa
kuitisha vikao vya kamati ya utendaji, Kuendesha klabu na kufanya maamuzi
binafsi bila ya kushirikisha kamati hiyo ya utendaji ambayo ilichaguliwa na
wanachama
Hivi karibuni klabu ya Simba ilizindua mchakato wa
kutengeneza mpango mkakati (Strategic Plan) lakini cha kushangaza mwenyekiti
amekuwa hataki kuona mpango huo ukifanikiwa.
Kushindwa kuitisha mkutano wa marekebisho ya katiba,kuchukua
maamuzi binafsi ya kuhairisha mkutano maalumu wa katiba uliotakiwa kufanyika
Novemba, mwaka huu.
http://www.shaffihdauda.com
0 comments:
Post a Comment