Home » » SIRI NZITO YAFICHUKA UJANGILI NCHINI .

SIRI NZITO YAFICHUKA UJANGILI NCHINI .

Jonh_Muya_af33b.jpg
(Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Kuhifadhi Wanyamapori nchini,Jonh Muya)
Wakati wanyama wakiwamo tembo wakiendelea kupotea kwa kuuawa kwa wingi na majangili katika hifadhi na mbuga mbqalimbali za taifa nchini, imeelezwa kuwa, wahalifu hao wamewekeza kwenye biashara hiyo haramu.
Akizungumza na NIPASHE jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Kuhifadhi Wanyamapori nchini, Jonh Muya, alisema majangili wamewekeza kwenye biashara hiyo haramu kama ilivyo kwa wale wanaojihusisha na dawa za kulevya, kwani imevuka mipaka ya nchi na mtandao wake ni mkubwa ndiyo maana imekuwa ikileta shida hata katika kukabiliana nayo.
Kwa mujibu wa Muya, matajiri ndiyo wahusika wakuu wa vitendo hivyo vya ujangili huku wakiwatumia walalahoi kwa ajili ya kuwachukulia mizigo yao kutoka kwenye hifadhi au mbuga za wanyama na kuipeleka maeneo walikoamriwa.
Akizungumzia tukio la kukamatwa kwa meno ya tembo takribani 1,000 Zanzibar mwanzoni mwa wiki iliyopita, Muya alisema tatizo hilo pia linaweza kuchangiwa na uwapo wa bandari bubu nyingi katika ukanda wa Bahari ya Hindi huku zikiwa hazina udhibiti maalumu.
Alisema kuanzia Bandari ya Tanga hadi ya Dar es Salaam kuna takribani bandari bubu 46, ambazo kwa namna moja au nyingine, hufanya udhibiti wa vitendo vya ujangili kuwa mgumu na kutokana na hiyo inawawia vigumu hata kujua bandari ipi ambayo meno hayo yalipitishwa hadi kwenda kukamatwa Zanzibar.
Alisema vita dhidi ya ujangili inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo ukosefu wa teknolojia ya kisasa katika kudhihiti uhalifu huo.
Hata hivyo, alisema wana mipango mbalimbali kwa ajili ya kukabiliana na vitendo hivyo ambavyo vinalenga kuliporomosha taifa kiuchumi kwa kukosa watalii, ikiwamo kuwa na vifaa vya kisasa kama boti na kushirikiana na nchi nyingine ili kupeana uzoefu wa namna wanavyokabiliana na ujangali kwenye nchi hizo.
 

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa