Home » » TAARIFA MUHIMU: DAWASCO KUZIMA MTAMBO WA RUVU CHINI 09/11/2013

TAARIFA MUHIMU: DAWASCO KUZIMA MTAMBO WA RUVU CHINI 09/11/2013



Shirika la Maji Safi na Majitaka Dar-es-salaam (DAWASCO), linasikitika kuwatangazia  wakazi wa jiji la Dar-es-salaam; Mji wa Bagamoyo kuwa Mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Chini utazimwa kwa wastani wa Saa 12 siku ya Jumamosi, Tarehe 09/11/2013 kuanzia saa 12 asubuhi hadi 12 jioni.

Mtambo wa Ruvu Chini utazimwa ili kuruhusu Mkandarasi  kuendelea na upanuzi wa mtambo

Kuzimwa kwa mtambo wa Ruvu Chini kutasababisha maeneo yafuatayo kukosa Maji:

MJI WA BAGAMOYO VIJIJI VYA ZINGA, KEREGE NA MAPINGA, BUNJU, BOKO, TEGETA, KUNDUCHI, SALASALA, JANGWANI, MBEZI BEACH NA KAWE.

Maeneo Mengine ni : MLALAKUWA, MWENGE, MIKOCHENI, MSASANI, SINZA, KIJITONYAMA, KINONDONI, OYSTERBAY, MAGOMENI, UPANGA, KARIAKOO, CITY CENTRE, ILALA, UBUNGO MAZIWA, KIGOGO, MBURAHATI, HOSPITALI YA RUFAA MUHIMBILI, BUGURUNI, CHANGOMBE NA KEKO.

WANANCHI MNASHAURIWA KUHIFADHI MAJI NA KUYATUMIA KWA MATUMIZI YA LAZIMA.

DAWASCO INAWAOMBA RADHI KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA.

IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO-MAKAO MAKUU

“DAWASCO TUTAKUFIKIA”

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa