Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » Tanzania Arts Group watembelea ofisi za Tone Multimedia Group

Tanzania Arts Group watembelea ofisi za Tone Multimedia Group

Tanzania Arts Group limefanya ziara katika ofisi za Tone Multimedia Group ambao ni wamiliki wa blogs za mikoa na radio ya mtandaoni kwa lengo la kujionea namna kampuni hii inavyofanya kazi za kidigitali.

Mwenyekiti wa kundi hilo Manuari Mruma ‘Mr Nzoke’ na wanakikundi wenzake, pamoja na kujionea shughuli za Tone pia lilionyesha vipande kadhaa vya maigizo na kueleza mipango yake ya baadae katika kuendeleza sanaa ya filamu na maigizo.

 
 Kundi la Tanzania Arts katika picha ya pamoja walipotembelea ofisi za Tone Multimedia
 


 Mhariri wa habari, Dotto Kahindi (wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa wanakundi hao

 Mwenyekiti wa kundi hilo Manuari Mruma ‘Mr Nzoke’ akiuliza jambo
 Mwandishi wa habari za burudani, Seki David akifafanua jambo kwa wageni hao
 Mmoja wa wanakundi akiigiza kama mtoto yatima anayeteswa na walezi wake

Tanzania Arts Group ni kundi changa la sanaa linalohitaji michango mingi  kutoka kwa wadau mbalimbali wa sanaa ikiwa ni pamoja na msaada wa mawazo, ushauri na ushirikiano ili kuboresha kazi yake.

Kwa wale wanaopenda kufanya kazi na wasanii wa kundi hilo wanaweza kufanya mawasiliano na mwenyekiti wa kundi hilo Mr. Nzoke kwa simu namba 0658450420 au 0767929474.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa