Wahitimu
wa Jeshi wa Zimamoto na Uokoaji wa kozi ya kuzima moto wa ndege
wakizima moto kwenye ndege bandia kabla ya mafunzo yao kufungwa na
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi. Maofisa na Askari
21 wa jeshi hilo walihitimu mafunzo hayo na kukabidhiwa vyeti katika
hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na wahitimu
na wageni waalikwa kabla ya kufunga mafunzo ya kozi ya uzimaji moto wa
ndege. Maofisa na Askari 21 walihitimu kozi hiyo na kutunukiwa vyeti
katika sherehe fupi ya kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini (CG),
Pius Nyambacha. Kulia ni Meja Generali Kapwani, Mkuu wa Kamandi ya Jeshi
la Anga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akimkabidhi zawadi ya
cheti mwanafunzi aliyefanya vizuri katika masomo darasani, Mohammed
Shomari (kulia). Akizungumza baada ya kuwakabidhi vyeti wahitimu 21 wa
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji waliomaliza mafunzo ya kozi ya kuzima moto
wa ndege, Waziri Nchimbi aliwataka wahitimu hao wawe wahadilifu katika
kazi zao wakiiheshimu kazi. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji nchini (CG), Pius Nyambacha. Tukio hilo lilifanyika jijini Dar
es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kikosi
cha gwaride la wahitimu kikitoa heshima mbele ya mgeni rasmi (hayupo
pichani) wakati wa sherehe yao ya kumaliza mafunzo ya kozi ya kuzima
moto wa ndege kwa maofisa na askari 21 wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
waliohitimu kozi hiyo jijini Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi ambaye aliyafunga mafunzo ya kozi hiyo
aliwataka wahitimu hao wawe wahadilifu katika kazi zao wakiiheshimu
kazi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini (CG), Pius Nyambacha,
akimshukuru Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi
(kulia) kwa kukubali wito wao wa kuja kuyafunga mafunzo ya Maofisa na
Askari 21 wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji waliohitimu mafunzo ya kozi ya
kuzima moto wa ndege. Waziri Nchimbi katika hotuba yake aliwataka
wahitimu hao wawe wahadilifu katika kazi zao wakiiheshimu kazi.
Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
0 comments:
Post a Comment