BONDIA
bora wa mwaka 2013,2014 katika uzito wa KG 63 Ibrahimu Class 'King
Class Mawe' ame saini mkataba wa kupambana na Cosmas Cheka Feb 8 mwaka
huu katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam.
Mara
baada ya kusaini mkataba huo wa kucheza raundi 10 za ubingwa wa Taifa
kg,60 amesema atafanya mazoezi ya kutosha kuhakikisha ana msambaratisha
mpinzani wake raundi za awali kwa kuwa alikuwa anachonga sana juu yake
mpambano
huo uliodhaminiwa na Promota Maarufu nchini Jay Msangi utakuwa na
msisimko wa aina yake kutokana na mabondia hao kuwa gumzo katika
ulimwengu wa masumbwi ndani na nje ya nchi ya tanzania
King
Class aliongeza kwa kusema kuwa nipo fiti nimejiandaa na ninasubili tu
kuvishwa ubingwa huo wa taifa kwani Cheka ana ujanja kwangu mbinu zake
zote nimesha zikamata
King Class Mawe anae nolewa na jopo la makocha wanao ongozwa na Habibu Kinyogoli 'Masta' Rajabu Mhamila 'Super D' Kondo Nasoro
Bondio
huyo amewashukulu wadau wa mchezo wa ngumi kwa kumuwezesha kuchaguliwa
kuwa bondia bora wa mwaka katika uzito wake kwa kuwapita mabondia
wengine wanne na yeye kuibuka kidedea katika kin'yan'gan'yiro hicho
0 comments:
Post a Comment