Mbunge wa jimbo la Temeke, Abass Mtemvu
Akizungumza wakati akikabidhi kwa uongozi milioni 67.5/- ambao
yametengenezwa na Chuo cha Ufundi (Veta) Chang'ombe kutokana na fedha
za mfuko wa jimbo hilo.
Alisema kukamilika kwa idadi hiyo ni mwanzo wa kuondokana na
tatizo la ukosefu wa madawati kwa shule za msingi na sekondari ndani ya
eneo lake.
Mtemvu, aliongeza kwamba yeye kwa kushirikiana na madiwani
wameandaa mkakati wa kuchangisha pesa ili shule zote ziwe na madawati ya
kutosha
Afisa elimu wa msingi wa Manispaaya Temeke, Honorina Mumba,
alimshukuru Mbunge huyo kwa kujikita katika elimu kwa kuhakikisha
matatizo mbalimbali yanapatiwa ufumbuzi.
Alisema madawati hayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa kuziba pengo
lilopo la ukosefu wa madawati kwa shule za msingi na wanatarajia kwa
nguvu zake pamoja na madiwani suala hilo litafikia mwisho.
SOURCE:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment