Home » » PSPF NA FLAVIANA MATATA FOUNDATION WAELEZA MAFANIKIO YA ZOEZI LA KUGAWA VIFAA VYA SHULE MKOANI PWANI

PSPF NA FLAVIANA MATATA FOUNDATION WAELEZA MAFANIKIO YA ZOEZI LA KUGAWA VIFAA VYA SHULE MKOANI PWANI

Mfuko wa Pensheni PSPF kwa kushirikiana na Flaviana Matata Foundation wakutana na waandishi wa habari kueleza mafaniko na changamoto walizoziibua wakati wa zoezi la ugawaji wa vifaa vya shule katika shule za msingi mkoani Pwani.

Wanafunzi 1000 wa shule za msingi wamenufaika na mradi huo ambapo shule zilizopata mgao huo pamoja na idadi ya wanafunzi kwenye mabano ni shule ya Msingi, Msinune (300) ya Wilayani Bagamoyo, Chanzige (280) ya Kisarawe na Kimanzichana (420) ya Mkuranga na kila mwanafunzi amepatiwa madaftari 12, kompasi ya mahesabu, kalamu tatu, penseli 2 na ufutio mmoja.
 Kutoka kulia ni Meneja wa mradi huo, Lusajo Mwaisaka, Mwanzilishi wa Flaviana Matata Foundation na Mwanamitindo Flaviana Matata, Afisa Mahusiano na Masoko wa PSPF, Hawa Kikeke na Afisa Mfawidhi wa PSPF Mkoa wa Pwani, Tumaini Uledi wakielezea mafanikio na changamoto wakati wa ugawaji wa vifaa vya shule kwa wanafunzi wa shule ya msingi mkoani Pwani.
Afisa Mahusiano na Masoko wa PSPF, Hawa Kikeke (katikati) akieleza mikakati ya mfuko huo katika kusaidia elimu ya msingi nchini wakati wa kuhitimisha zoezi la ugawaji wa vifaa vya shule kwa wanafunzi wa shule ya msingi mkoani Pwani.
 Meneja wa mradi wa back to school, Lusajo Mwaisaka akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam, kushoto kwake ni Mwanzilishi wa Flaviana Matata Foundation na Mwanamitindo Flaviana Matata na Afisa Mahusiano na Masoko wa PSPF, Hawa Kikeke

 Kutoka kulia ni Mwanzilishi wa Flaviana Matata Foundation na Mwanamitindo Flaviana Matata na Afisa Mahusiano na Masoko wa PSPF, Hawa Kikeke wakionyesha baadhi ya vifaa kwa waandishi wa habari.

PICHA NA BLOG ZA MIKOA

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa