Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe
Walitoa lawama katika kikao kilichoitishwa jana na Waziri wa
Uchukuzi, Dk. Mwakyembe, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuzungumzia
changamoto zinazoikabili bandari na idara zote zinazofanya kazi katika
bandari hiyo.
Walimweleza Dk. Mwakyembe kuwa kampuni ya TICTS imekuwa
ikichelewesha utoaji wa makontena ya wateja bandarini katika kipindi cha
siku 15 ambazo zipo kisheria na baada ya hapo mteja anaambiwa atoe
gharama ambazo ni Dola za Marekani 100.
Walisema wateja wanatozwa kiwango hicho na TICTS bila kujali kuwa
mfumo wa ufuatilia wa mizigo ujulikanao kama "Cargo Management System"
ulioanzishwa na TRA umegoma kufanya kazi jambo ambalo linawawia vigumu
katika utendaji kazi.
“TICTS wanachelewesha makontena kwenda bandarini na mteja
analazimika kulipa gharama za kutunza mzigo ambazo kama kontena
lingeweza kutolewa ndani ya siku 15 baada ya kuwasili kutoka nje mteja
asingeweza kuingia gharama hizo,” walisema.
Wadau hao pia waliitupia lawama TRA kutokana na mfumo wake mpya wa
ufuatiliaji mizigo bandarini kuwa na usumbufu kutokana na wakati
mwingine kushindwa kufanya kazi hadi siku saba.
Walisema hali hiyo imekuwa ikisababisha wateja hususani wanaotoka
nje ya nchi kuingia gharama kubwa wakisubiri mizigo yao kutoka bandarini
na mwisho wa siku wanalazimika kukimbia kuitumia bandari ya Dar es
Salaam na kukimbilia bandari nyingine ambazo hazina urasimu.
Meneja kituo wa TICTS, Donald Talawa, alisema tatizo la
ucheleweshaji wa makontena bandarini limetokana na ongezeko la mizigo
kutoka makontena 600 hadi kufikia 800 katika kipindi cha Desemba mwaka
jana na hivi sasa kampuni imejipanga kutatua tatizo hilo.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment