Siku
kadhaa zilizopita kupitia millardayo.com kuna taarifa ziliztoka kuhusu
kufungiwa kwa video ya Nimevurugwa ya Snura,taaarifa hizi alizi-amplify
meneja wake Snura ‘Hk’ akidai kuwa sababu maalum bado hawajazipata
ingawa kila kituo anachoenda wanampa sababu tofauti.
Millardayo.com
haikuishia hapo ilienda moja kwa moja kwenye Baraza la Sanaa la
Taifa(Basata)ili kuujua undani wa sakata hili ikiwemo pia kuulizia video
ya Jux(uzuri wako)ambayo nayo ilitoka taarifa ya kufungiwa kwa video
hiyo.
Kutoka
Basata huyu hapa Godfrey mungeleza ni kaimu katibu mtendaji anataarifa
zaidi>>Unaposema kufungia video moja kwa moja kuna chombo kingine
cha serikali kinashughulikia hilo ambao ni bodi ya filamu Tanzania’
‘Bodi ya
filamu wanaangalia video zote suala zima la filamu wanapoona hii
haikidhi au haifai kwa jamii za Kitanzania basi wanaisimamisha kidogo
wanamshauri aweze kuirekebisha ili iweze kulingana na maadili ya
kitanzania’
‘Sisi
tunaangalia Audio kabla haijaingia sokoni katika urasimishaji tunakaa
tunausikiliza muziki wake tunashauriana kwamba akarekebishe hapa na
tunaangalia mambo mengi ikiwemo ubunifu wake mwenyewe’
‘Suala
la kufungiwa kwa Snura najua kabisa linaenda kwenye suala la maadili na
limeandikwa sana na sisi Baraza kama Baraza tunaangalia sana suala la
maadili tukisema tunamfungia hatufungii video tu tunamfungia msanii
mwenyewe’
Bonyeza play kumsikiliza Kaimu Katibu mkuu akielezea suala hili.
0 comments:
Post a Comment