Home » » JIJI MNALIONA HILI: DAMPO LISILO RASMI LAHAMIA KITUO CHA KUPAKIA BAJAJI MWENGE.

JIJI MNALIONA HILI: DAMPO LISILO RASMI LAHAMIA KITUO CHA KUPAKIA BAJAJI MWENGE.

Eneo la Mwenge ambapo Kuna kituo kikubwa cha Bajaji kimegeuka kuwa Dampo la kutupia matakataka jambo lililosababisha kero kubwa kwa wananchi wanaopita katika eneo hilo na ofisi za jirani kutokana na Harufu mbaya ambayo inatokea hapo, wakati Jiji wanaliona hilo na wanalifumbia macho Dampo hilo lisilo Rasmi.

Wenyeji wa eneo hilo wakiwemo madereva wa Bajaji wamesema kuwa kuna tatizo kubwa la kutupa takataka hizo likiongozwa na wafanya usafi wa jiji ambao wanatoa taka kutoka barabarani na Mitaroni kisha kuzitupia hapo, wameongeza kuwa kuna vibanda vingi vya mama Antilie ambavyo kwanza ni vichafu na vipo katika mazingira hatarishi nao wanatupia taka zao katika eneo hilo na kundi la mwisho ni wale mafundi wa Bajaji nao wanatupia taka zao hapo.
Hata hivyo wananchi wanaoishi katika eneo hilo wameiomba Halmashauri ya jiji kuwawekea Dampo ili waweze kutupa takataka hizo kwa utaratibu na kuepusha 

Hili ni Dampo lisilo Rasmi ambalo lina taka taka za kila aina zinazosababisha usumbufu kwa Kutoa harufu mbaya, Mbele kidogo vinavyo onekana ni vibanda vya mama Antilie ambavyo vipo jirani kabisa na Dampo hilo, jambo ambalo ni Hatarishi kwa afya za wakazi wa eneo hilo.

Taka taka za kila aina zikiwa zimerundikana katika Dampo hilo

 Hali halisi ya Dampo hilo lisilo Rasmi..

 
 
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa