Home » » ‘Mbwa mwitu’ wakamatwa

‘Mbwa mwitu’ wakamatwa

POLISI jijini Dar es Salaam, wamewakamata vijana 169 wanaojiita ‘mbwa mwitu’ au ‘watoto wa mbwa.’ Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema makundi hayo ya vijana yalikamatwa katika mikoa ya kipolisi ya Temeke, Ilala na Kinondoni. Kwa mujibu wa Kova, baada ya opereheni hiyo ya polisi, vijana hao walikimbilia katika maeneo ya nje ya mji.
"Vijana hao sio wasomi, hawana kazi yoyote hivyo kazi yao ni kuzurura na kuunda vikundi vya kukaba watu na kupora vitu mbalimbali.

"Kuanzia leo nimetoa wiki moja sitaki kusikia habari ya mbwa mwitu au watoto wa mbwa, waliopo katika maeneo hayo.

"Nimewaagiza makamanda wakuu wa mikoa yote, kufanya operesheni maalumu ya kuingia nyumba hadi nyumba, kwa ajili ya kuwasaka vijana wanaojihusisha na vikundi hivyo," alisema Kova.

Wakati huo huo, polisi imekamata pikipiki 150 kwa lengo la kudhibiti vitendo vya uhalifu, kwa kutumia usafiri huo .

Kova alisema operesheni hiyo inahusisha kikosi kazi kinachojumuisha askari mbalimbali, wakiwamo wale wenye sare, usalama barabarani, askari wa upelelezi na vikosi vingine vya kulinda usalama.

Operesheni hiyo ilianza Januari 28, mwaka huu, ambayo ilifanyika kwa kanda za mikoa ya kipolisi ambayo ni Ilala, Temeke na Kinondoni.

Alisema baadhi ya pikipiki zimetozwa faini na nyingine kuachiwa huru, baada ya kuonekana hazina upungufu huku nyingine zikiendelea kushikiliwa kwa mahojiano zaidi.

Chanzo;Mtanzania 

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa