Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),
Balozi Fulgence Kazaura (74), unatarajiwa kuwasili nchini leo ukitokea
Chennai, India alikokwenda kwa matibabu ya saratani.
Makamu Mkuu wa Chuo cha UDSM, Profesa Rwekaza
Mukandala alisema jana kuwa, mwili huo utawasili alasiri kwa ndege ya
Shirika la Ndege la Emirates na kesho kutafanyika misa ya kumwombea
katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Peter, Oysterbay kuanzia saa 7.00
mchana.
Profesa Mukandala alisema keshokutwa watatoa
heshima za mwisho na kutakuwa na sherehe ya kumuaga katika Ukumbi wa
Nkurumah ulioko UDSM kuanzia saa 8.00 mchana.
Balozi Kazaura alifariki Jumamosi iliyopita nchini India.
Alisema Ijumaa asubuhi, mwili wa Balozi Kazaura
utasafirishwa kwenda kijijini kwao Kijumo Misenyi Mkoa wa Kagera kwa
mazishi yatakayofanyika Jumamosi.
Marehemu aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam kwa zaidi ya muongo mmoja na mkuu wa chuo hicho
kwa kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2005 hadi mauti yalipomfika.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment