Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, inatarajia
kuchunguza kwa kuzifanyia uhakiki mali za viongozi 300 katika mwaka wa
fedha wa 2013/14.
Lengo likiwa ni kutathmini matamko ya rasilimali na madeni yaliyowasilishwa.
Akizungumza hivi karibuni, Kamishna wa
Sekretarieti hiyo, Jaji mstaafu Salome Kaganda aliwaeleza wajumbe wa
Kamati ya Katiba na Sheria kuwa, wanatarajia kuanza kazi hiyo Machi
mwaka huu baada ya kupokea fedha zilizotengwa kwa kazi hiyo.
“Baadhi ya matamko hayatolewi kwa ukamilifu, kwa
mfano kutotaja thamani halisi ya mali hizo, wala sehemu zilipo na jinsi
zilivyopatikana na kusita kutaja namba za akaunti za benki na kiwango
cha fedha kilichopo,” alisema Jaji Kaganda na kuongeza:
“Pia, kushindwa kutaja mali za mke au mume na watoto walio chini ya miaka 18.”
Jaji Kaganda alisema kumekuwa na changamoto kubwa
kwenye ujazaji matamko, viongozi wengi wamekuwa wakichelewa ku wakilisha
kama inavyotakiwa Desemba 31 kila mwaka.
“Desemba viongozi wa siasa waliorejesha matamko
walikuwa 3,081 sawa na asilimia 76 ya 4,971, wakati viongozi wa utumishi
wa umma waliorejesha ni 5,319 kati ya 8,148, hivyo hali ya urejeshaji
ilikuwa ni mbaya kutokana na viongozi wengi kutokamilisha hasa
watumishi,” alisema.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment