Katibu
mkuu wizaraya Nishati na Madini, Eliakim Maswi (Watatu kushoto),
akizungumza jambo na Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Nishati na Madini,
Victor Mwambalaswa (Wanne kushoto), wakati kamati hiyo ilipotembelea
bandari ya Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kujionea kazi ya upakuaji
vifaa vya ujenzi na kupokea shehena ya mwisho ya mabomba ya kupitishia
gesi. Wengine ni wajumbe wa kamati hiyo, Raha Mohammed (Kulia), Richard
Ndasa (Wapili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya
Petroli nchini (TPDC), Yonah Kilagane.
Katibu
Mkuu wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi (Wapili kushoto),
akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini,
ikiongozwa na mwenyekiti wake, Victor Mwambalaswa (Wakanza kushoto)
kuhusu kazi ya upakuaji vifaa vya ujenzi na kupokea shehena ya mwisho ya
mabomba ya kupitishia gesi bandarini jijini Dar es Salaam mwishoni mwa
wiki. Watatu kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli
nchini (TPDC), Yonah Kilagane.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Victor Mwambalaswa
(Wapili kulia) na mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, Mhe Richard Ndasa,
wakiangalia kazi ya upakuaji saruji kutoka kwenye meli bandarini jijini
Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kamati hiyo ilitembelea ili kujionea
kazi hiyo na ile ya kupokea shehena ya mwisho ya mabomba ya kupitishia
gesi kutoka Mtwara kuja Dar es Salaam.
TANZANIA inatarajia
kufaidika na matumizi ya gesi asilia ambayo yataokoa zaidi ya shilingi Trilioni 1.6trn/- kila mwaka, mara baada ya
gesi ya Mtwara kuanza kutumika katika sekta mbalimbali, mara kazi ya ujenzi wa bomba la gesi
toka Mtwara kuja jijini Dar es Salaam itapokamilika.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya
Nishati na Madini Mhe. Victor Mwambalaswa (mb) wakati wa hafla ya kupokea
shehena ya mwisho ya mabomba kwa ajili ya ujenzi wa bomba la gesi asilia kutoka
Mtwara na Songo Songo hadi Dar es S.alaam.
Mhe. Mwambalaswa amesema, kiasi hicho cha fedha ndicho
kinachotumika na taifa kuagiza mafuta ya kuendesha mitambo mbalimbali ambapo
baada ya gesi kufika Dar es Salaam, fedha hizo sasa zitaelekezwa kwenye maeneo
mengine kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania.
Mhe. Mwambalaswa amesema utekelezaji wa mradi utaleta manufaa
makubwa kwa wananchi hasa maeneo gesi asilia inapopatikana. Huduma mbali mbali
za jamii kama vile maji, umeme, afya, elimu na miundombinu zitatolewa au
kuboreshwa. Mapato ya kodi za Halmashauri yataongezeka na ajira kwa wazawa
zitaongezeka.
Akimkaribisha
mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini, Bw. Eliakimu Maswi,
alizitaja baadhi ya faida ambazo
wananchi wa Mtwara na Lindi watafaidika nazo ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa
mitambo ya kusafishia gesi itakayojengwa Madimba na Songo Songo: Kila mtambo
utahitaji kiasi cha wafanyakazi wa moja kwa moja wapatao sitini (60)
watakaoendesha mitambo hiyo. Vile vile, kutahitajika watu watakaotoa huduma ya
chakula, afya, usafiri pamoja na huduma nyingine za kijamii.
Bw.
Maswi ameelezea kuhusu ujenzi wa kiwanda cha saruji cha kampuni ya Dangote
ambacho kitatoa ajira rasmi kwa wananchi takribani 500 na zile zisizo rasmi
takribani watu 800 na ujenzi wa kiwanda kingine cha Saruji cha kampuni ya Meis
kitakatoa ajira kwa wananchi takribani 1000.
Bw,
Maswi amesema, wizara yake ya Nishati na Madini imetenga fungu maalam ambalo
litatumika kuwapatia umeme wananchi wa vijiji vyote vinavyopitiwa na bomba gesi.
Sambamba
na faida hizo za jumla, pia sehemu ya gesi itakayozalishwa katika maeneo ya
Mnazi Bay, Ntorya na kina kirefu cha maji itaendelea kutumika kuzalisha umeme
kwa matumizi ya mikoa ya Mtwara na Lindi pamoja na mikoa mingine inayopakana
nayo, wakati kwenye matoleo ya bomba la kusafirisha gesi limeweka matoleo ya
kuchukulia gesi asilia (off take) katika miji ya Mtwara, Lindi, Kilwa na
Mkuranga ili kuhakikisha kuwa maeneo haya yanapata gesi asilia ya uhakika kwa
ajili ya viwanda na matumizi mengine.
Nae
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini, Bw. Yona Kilaghane, amesema
mazungumzo ya ujenzi wa mitambo ya (LNG) yameanza kati ya TPDC, kupitia Wizara
ya Nishati na Madini na Makampuni ya Statoil, British Gas (BG), Ophir pamoja na
Exxon Mobil ili kuzalisha LNG kwa kutumia mtambo mkubwa utakaojengwa karibu na
maeneo ya ugunduzi.




0 comments:
Post a Comment