Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Angels Moment, Bi Naima Malima (kushoto) akimkabidhi zawadi Mgeni Rasmi wa Tamasha hilo, Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilali wakati wa Ufunguzi wa Tamasha hilo,ulioanza rasmi leo katika Ukumbi wa DarLive,Mbagala jijini Dar es Salaam.
Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pesheni PPF,Lulu Mengele akipokea tuzo ya udhamini kutoka kwa Mke wa makamo wa Rais Mama Asha Bilali katika tamasha la Mwanawake weka akiba,leo jijini Dar es salaam.
Mke wa makamu wa Rais Mama Asha Bilali ambaye alikuwa mgeni rasmi wa Tamasha la Mwanawake weka akiba, akisoma hotuba ya ufungunzi wa tamasha hilo,leo jijini Dar es salaam katika viwanja vya Dar live Mbagala.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akitoa ushuhuda wake juu ya kutumia fursa katika ujasiriamali. Mama Tunu alishiriki katika Tamasha hilo akiwa mjasiriamali aliyekuwa akiuza mazao yatokanayo na nyuki.
Mkurugenzi Mkuu wa Angles Moments Naima Malima akisoma risala ya kumkaribisha mgeni rasmi Mke wa Makamo wa Rais, Mama Asha Bilali katika ufunguzi wa tamasha la Mwanawake weka akiba litakalofanyika kwa siku tatu katika viwanja vya Dar live Mbagala.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akimuonesha bidhaa zilizomo bandani kwake alipotembelewa na Mgeni Rasmi wa Tamasha hilo, Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilali.
Baadhi ya kina mama waliojitokeza kuhudhuria Tamasha hilo.
burudani kutoka THT, ambao waliigiza mahudhui ya Tamasha.
Wake wa Viongozi (New Millenium Women Group) wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi wa Tamasha hilo, Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilali.
********
********
Na Mwandishi wetu
Wanawake
nchini wameaswa kujenga tabia ya kutunza akiba ili kufikia malengo
wanayojiwekea na kwa maendeleo ya familia zao.
Wito huo umetolewa na Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilali wakati
akifungua Tamasha la kwanza la kipekee kwa ajili ya wanawake na vijana
lililopewa jina la Mwanamke na Akiba na linalofanyika kwa muda wa siku
tatu jijini, Dar es Salaam.
Mama
Asha alisema kuletwa kwa Tamasha hilo ni fursa mojawapo na adimu sana
kwa wanawake kujipatia utaalamu na kupanua wigo wao kibiashara.
Alisema
kuwa maendeleo ya Tanzania yanaanza kwa kina mama kwa wao wenyewe
kujijengea tabia ya kujiwekea akiba japo kidogo ni kwani ni furaha na
mkombozi wa siku za baadae.
“Akiba
ni msingi wa maendeleo ya kila mwananchi. Kwa kila biashara, na kila
ajira tuliyonayo, bila kuwa na elimu na utaratibu wa kujiwekea akiba
tutazidi kuwa na kipato kidogo hivyo kushindwa kuendelea kiuchumi na
kijamii,” aliasa Mama Asha.
“Nachukua
nafasi hii pia kuwaomba wanawake wote watakaohudhuria kutilia maanani
mafunzo yote watakaopewa katika siku mbili zijazo ili kuweza kujenga
uwezo wao katika uwekaji wa akiba,” aliongeza.
Mama
Asha aliipongeza kampuni ya Angels Moment pamoja na timu yake kwa
kuwaza kuandaa tamasha hilo la elimu kwa akina mama hususani walio
katika sekta isiyo rasmi kwani linatoa fursa ya kuwatoa wanawake katika
utegemezi na umaskini kwa kuongeza kipato chao.
Nae,
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Angels Moment, Bi Naima Malima alisema
lengo kuu la Tamasha hilo ni Kuboresha kasumba ya kujiwekea akiba,
hususan ikwa akina mama, na mbinu mbalimbali za kujiongezea kipato
miongoni mwao.
“Tamasha
hili limeandaliwa ili kuwaonesha wanawake na vijana umuhimu wa kuweka
akiba, aina tofauti za kuweka akiba na njia mbalimbali za kuweka akiba
pamoja na fursa za kuweka akiba kimkakati kupitia uwasilishaji wa mada
na maonesho,” alisema Bi Naima.
Aliongeza
kuwa washiriki watapata fursa ya kupata elimu juu ya kukabiliana na
hatari katika uhifadhi wa fedha na masuala mbalimbali yahusikanayo na
usimamizi wa fedha.
“Tamasha
linatoa fursa za maonyesho na semina ambazo zitawaelimisha wanawake
namna tofauti za kuweka akiba, na mbinu mbalimbali za kujikimu,” alisema
Bi Naima.
Aliongeza
kuwa Tamasha hili pia linakusudia kuwaelimisha wanawake umuhimu wa
kuweka akiba, mbinu tofauti za kuweka akiba na jinsi ya kukabiliana na
changamoto mbalimbali katika kujiwekea akiba.
Tamasha
hilo linalofanyika katika Ukumbi wa Dar Live - Mbagala, jijini Dar es
Salaam limehudhuriwa na mamia ya kina mama na vijana ikiwemo wake wa
viongozi waliongozwa na Mama Tunu Pinda ambaye ameshiriki kama
mjasiriamali wa kuuza mazao ya nyuki.
0 comments:
Post a Comment