Mkurugenzi wa mamlaka ya mawasiliano (TCRA) Profesa John Nkomo
Kutoka kulia ni Pro.Nerey Mvungi katikati ni Dr.francis sichona mtaalamu wa Takwimu kushoto ni Mr.F.M Ishengoma mtaalam wa Habari na mawasiliano
waandishi wa habari wakiwa katika mkutano wa tathimini katika jengo la (TCRA)
Mtaalam wamawasiliana ya ki electronic Pro.Nerey mvungi
kaim naibu mkurugenzi Endrew kisaka kulia akiwasambambana
Meneja wa mawasiliano (TCRA) Innocent mungi
Habbi Gunze mkurugenzi wa utangazaji (TCRA)
Endrew kisaka kaim naibu mkurugenzi utangazaji
Tathimini ya uzimwaji wa mitambo katika kuelekea dijitali na
mamlaka ya mawasiliano Tanzania umekamilika ambapo (TCRA) iliweza kuunda jopo
la watu watatu katika kufanikisa tathimini hiyo ambao ni wataalamu toka chuo
kikuu ,ambapo tathimini hiyo imejengwa katika maeneo makuu matatu .
Eneo la kwanza likiwa ni Tathmini ya utendaji na utoaji huduma
za utangazaji kwenye mfumo wa kidijiti ikiwa ni pamoja na usimikaji wa miundo
mbinu ya kidijiti,na eneo la pili ni katika Tathmini ya kuangalia jinsi Mamlaka
ya Mawasiliano ilivyokuwa imejizatiti kuandaa na kusimamia zoezi zima la
uhamaji toka mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda kidijiti, eneo la tatu ni
watumiaji wa huduma za utangazaji walivyopokea mabadiliko hayo na changamoto
zilizopo na eneo la nne na mwisho ni zoezi zima la uzimaji mitambo
lilivyoendeshwa.
Jopo
hilo lilieleza Mambo ambayo walizingatia katika uzimaji uzimaji wa mitambo kwa
awamu ya kwanza katika mikoa saba moja wali hakikisha kuwepo kwa idadi ya soko
la visimbuzi kabla mitambo haijazimwa,idadi ya watu walio weza kununua ,elimu
kwa wadau wakati wa mchakato wa uzimaji mitambo,ubora wa visimbuzi na upokeaji
matangazo
Vivyohivyo
jopo hilo lili ainisha njia iliyo tumika katika kufanya tathimini kuwa ni ile
njia inayo tumika kimataifa kuendesha
mazoezi kama haya ijulikanayo kama “Sampling Approach” ambapo takwimu hukusanywa
kwa kuzingatia uwiano wa kaya zilizopo kwenye eneo husika, jinsia, umri, elimu
na kazi za kumuingizia kipato mtu anayehojiwa, Makundi mabalimbali yanayohusika
kwenye mchakato huu wa uhamaji kutoka mfumo wa analojia kwenda dijitali
yalihojiwa kwa kupitia dodoso maalumu lililoandaliwa na maoni yao yalikusanywa
Baada
ya jopo la wataalamu wa Chuo Kikuu kukaa na kufanya tathimini waliamua kutoa
matokeo ya tathimini hiyo kama ifuatavyo
1.
Katika
utendaji na utoaji huduma za utangazaji katika mfumo wa kidijitali na USIMIKAJI WA MIUNDO MBINU YA KIDIJTI.
(a)
Asilimia
89% ya kaya za watumiaji (consumers) walikuwa wakitumia huduma ya matangazo kwa
mfumo wa kidijiti mara baada ya uzimaji wa mitambo ya analojia kwenye miji saba
ambayo tathmini ilikuwa ikifanyika
(b)
Asilimia
11% ya kaya za watumiaji hawakuweza kupokea matangazo ya kidijiti kwa sababu
mbalimbali kama ifuatavyo:-
-
5.5%
hawakununua visimbuizi
-
0.1%
ya Kaya, walisema visimbuzi vilikuwa havipatikani
-
3.2%
ya Kaya, walishindwa kunua visimbuzi sababu ya bei kuwa juu
-
0.2%
ya Kaya visimbuzi vyao vilikuwa vibovu
-
0.3%
ya Kaya, visimbuzi havikuweza kupokea matangazo ya kidijiti kwa sababu ya
mawimbi hayapatikani kwa ubora zaidi (Poor signal reception)
-
0.9%
ya Kaya Luninga (TV screen) zilikuwa mbovu
-
0.7%
ya Kaya hawakuwa na umeme
2. UTAYARI
WA MAMLAKA YA MAWASILIANO KUANDAA NA KUSIMAMIA ZOEZI ZIMA LA UHAMAJI TOKA
UTANGAZAJI WA MFUMO WA ANALOJIA KWENDA KIDIJITI
- Jopo la wataalamu lililokuwa likiendesha tathmini hii
liliweza kuthibitisha kuwepo kwa baadhi ya nyaraka kutoka Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikiwa ni Kuwepo kwa kamati ya Kiufundi inayoundwa
na wadau mbalimbali, dira madhubuti inayoonyesha mambo muhimu ya kutekelezwa, sheria
na kanuni zinazosimamia zoezi la uhamaji toka analoja kwenda kidijiti,
Vilevile Jopo la wataalamu liliweza
kuthibitisha mambo yafuatayo:-
Muundo
bora wa leseni unaozingatia utoaji huduma za matangazo ya kidijiti, Utaratibu
mzuri wa ushindani kwa njia ya wazi uliotumika kuwapata “Multiplex Operators”
(wajenga Miundombinu na Wsambazaji wa matangazo), Utaratibu mzuri wa ushindani
kwa njia ya wazi uliotumika kuwapata “Multiplex Operators” (wajenga Miundombinu
na Wsambazaji wa matangazo) na mengine mengi
3. MATOKEO
YA TATHMINI KUHUSU UPATIKANAJI WA VISIMBUZI NA ELIMU KWA UMMA
Tathmini
imeonyesha kuwa kati ya kaya zote zilizohojiwa kwenye miji saba, ni 0.1% ya
kaya zilizodai uhaba wa visimbuzi wakati wa zoezi zima la uzimaji mitambo ya
analojia
4. ZOEZI
LA UZIMAJI MITAMBO YA ANALOJIA
Ilifahamika
kuwa zoezi la uzimaji mitambo ya analojia lilifanyika kwenye awamu nne ambapo
kila awamu ilitoa nafasi ya mwezi mmoja. Jopo la wataalam limeridhika na
utaratibu huu, ambao unatoa nafasi kubwa ya kutathmini matatizo yanayojitokeza
kwenye awamu ya kwanza kabla ya kwenda kwenye awamu nyingine. Vilevile ulitoa
fursa ya kuhakikisha kuwa eneo linalofuata linakuwa na visimbuzi vya kutosha na
elimu kwa umma inatolewa kikamilifu kwa kutumia Radio na Televissheni za eneo
husika.
5. WATENGENEZAJI
NA WASAMBAZAJI MAUDHUI (CONTENT SERVICE PROVIDERS)
65% ya watengenezaji na wasambazaji
wa maudhui walikuwa wamejiunga na mfumo wa kidijiti kabla ya uzimaji wa mitambo
ya analojia.
Sababu kubwa ya vituo vingine
kutojiunga na mfumo huu kwa wakati ilikuwa ni sababu za kimazoea kwamba huenda
mitambo isingezimwa kwa wakati uliopangwa. Mpaka sasa vituo vyote vilivyopo Dar
es Salaam vimeshajiunga na mfumo huu kasoro kituo kimoja.
6. MAJUMUISHO
Jopo
la wataalam limeridhika kuwa watazamaji wengi waliokuwa kwenye mfumo wa
analojia walijiunga kwenye mfumo wa kidijiti. 11% tu ndio ambao hawakuweza
kujiunga kwa sababu mbalimbali kama nilizoelezea mwanzoni. Idadi hiyo inaweza
kuwa imepungua kwa vile watu wamekua wakiendelea kununua visimbuzi,
Kutokana
na matokeo ya tathmini iliyofanyika serikali inashauriwa iendelee na zoezi la
uzimaji mitambo ya analojia sehemu zilizobakia. Jopo limeridhika na uandaaaji
na usimamizi wa zoezi hili na kwamba kasoro zilizojitokeza ni sababu ya hofu ya
mabadiliko na uzoefu wa walaji kwenye matumizi ya visimbuzi. Vilevile kuna
faida nyingi za mfumo wa kidijiti ambazo watoa huduma wanatakiwa kuzitumia ili
kuchochea ukuaji wa uchumi nchini.
Serikali
inashauriwa kutoa punguzo la kodi kwa visimbuzi ili kuwawezesha watanzania
wengi zaidi kununua visimbuzi na kupata habari kwa njia ya Luninga
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment