Ufisadi
mkubwa kupitia sekta ya afya umebainika katika Manispaa ya Kinondoni,
jijini Dar es Salaam, ambayo inadaiwa kutumia mamilioni ya shilingi kwa
matumizi hewa yanayohusisha upanuzi wa chumba cha kuhifadhi maiti,
kununua vifaa vya wodi ya wazazi na huduma ya usafiri wa wafanyakazi,
katika hospitali mbalimbali zilizoko katika manispaa hiyo.
Majina ya hospitali, ambazo zimetajwa kutumiwa na baadhi ya maofisa wa manispaa hiyo ‘kutafuna’ fedha hizo katika mwaka wa fedha 2011/2012, ni Mwananyamala, Magomeni na Sinza Palestina.
Ufisadi huo ulifichuliwa na timu iliyoundwa kupitia mikutano ya wananchi katika kata zilizoko katika manispaa hiyo, kwa ajili ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (Sam), kupitia ripoti yake iliyowasilishwa katika mkutano wa wadau wa afya katika manispaa hiyo, jijini Dar es Salaam jana.
Mchakato wa timu hiyo, ambao uliwezeshwa na shirika lisilo la kiserikali la Sikika, ulifanywa kwa lengo la kuijengea uwezo jamii kufanya chambuzi za taarifa mbalimbali pamoja na kufuatilia utekelezaji wa mipango na miradi inayotekelezwa na serikali.
Mjumbe wa timu hiyo, Samwel Mhando, akiwasilisha ripoti alisema ripoti ya manispaa ya utekelezaji inaeleza kuwa kuna upanuzi wa chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Mwananyamala ili kichukue maiti 50 badala ya 15, lakini hakuna upanuzi wowote uliofanyika wakati fedha inaonekana imetumika.
Mhando alinukuu moja ya vitabu vya ripoti ya manispaa na kusema fedha zinazodaiwa kutumika kwa ajili ya upanuzi wa chumba hicho ni Sh. milioni 30.
Alisema pia mpango na ripoti ya utekelezaji ya manispaa vinasema kuna fedha zimetumika kwa ajili ya vifaa katika wodi ya wazazi ya Hospitali ya Magomeni, wakati katika hospitali hiyo hakuna wodi hiyo.
Alisema ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa fedha zilizopangwa kwa ajili ya usafiri wa wafanyakazi wa Hospitali ya Sinza Palestina zimetumika zote, lakini Mganga Mfawidhi wa hospitali hana usafiri na wala hakupata posho za usafiri.
Alisema timu ilibaini changamoto nyingi katika vituo vya afya katika manispaa hiyo, ikiwamo mbao za matangazo kutokuwa na taarifa za mapato na matumizi ya kituo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Celestine Onditi, akifunga mchakato wa timu hiyo uliofanyika katika vituo 36 vya afya katika manispaa hiyo, aliipongeza Sam pamoja na Sikika kwa kazi nzuri waliyoifanya na kuwaomba waendelee kuishauri zaidi serikali ili huduma za afya zinazotolewa zitumike kwa kiwango kinachofaa.

CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment