Home » » Exim: Wekeni fedha benki

Exim: Wekeni fedha benki

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Meneja Uhusiano wa Biashara wa Benki ya Exim Tanzania, Justin Wambali (kushoto) akizungumza na mteja aliyetembelea banda la benki hiyo, wakati wa maonyesho ya biashara ya siku nne na mkutano wa Kibiashara na uwekezaji uliojumuisha wadau kutoka Israel na Tanzania unaoendelea jijini Dar es Salaam

Benki ya Exim Tanzania imewashauri wananchi kutumia huduma za fedha za kibenki kwa ajili ya usalama na maendeleo yao.
Wito huo ulitolewa jana na Meneja Uhusiano wa Kibiashara wa Exim, Justin Wambali wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku nne wa kibiashara na uwekezaji uliojumuisha wadau kutoka Israel na Tanzania.
Mkutano huo uliambatana na Maonyesho ya Biashara ya Tanzania- Israel  Business  and Investment Forum (TIBIF), yanayoendelea jijini Dar  es Salaam.
Akizungumzia mkutano wa TIBIF uliofunguliwa na Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal alisema, umekutanisha wadau  kutoka taasisi za kibiashara na uwekezaji zinazojishughulisha na kilimo, madini, huduma za fedha, elimu,miundombinu (barabara, maji), ujenzi na makazi.
Mkutano huo umewakutanisha wadau zaidi ya 500 kutoka sekta za biashara, wawekezaji, watunga sera, viongozi katika viwanda  na watoa uamuzi kutoka kampuni mbalimbali na taasisi nyingine.
Chanzo;Mwananchi

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa