Mtandao wa pamoja Blog ilifanikiwa kumnasa kijana mmoja wa mtaani
ambaye alikuwa anaosha vioo vya magari kwenye foleni ya makutano ya
barabara ya Morroco road, Alli Hassan Mwinyi, Mwai Kibaki na Barabara ya
Bagamoyo akiwa hana hata shati na mvua ilikuwa ikinyesha. Hii
ilionekana kama ni kuhatarisha maisha yake kwani magari yakiruhusiwa
anaweza kugongwa na licha ya ilo afya yake inaweza kuwa mbaya zaidi.
Kijana
huyo akielekea kwenye gari mojawapo lililokuwa liko kwenye foleni kwa
ajiri ya kulisafisha kioo cha gari. Na pia barabara hii inatumiwa na
viongozi mbalimbali wa kitaifa inamaana hawaoni vijana hawa maana eneo
hili kuna watoto wenye umri wa miaka minne na wanafanya kzi hizi za kuosha vioo vya magari.
Kijana huyu akisafisha kioo cha moja ya magari yaliyokuwa kwenye foleni hiyo.
Selikari
isipoona tatizo hili watakao umia zaidi ni wananchi maana kwa hali kama
hii tunatengeneza bomu kubwa ambalo litalipuka vibaya kwani ndani ya
hawa watoto ndo wanazaliwa majambazi na hata vibaka
Akimalizia
kusafisha kioo hicho cha gari na alipomaliza kusafisha alielekea upande
wa dereva na kupewa shilingi mia tano za kitanzania.
Baada
ya taa za kuongozea magari ziliporuhusu kwenye barabara ya Ali Hassan
Mwinyi alianza kupishana na magari ili kufika katikati ya barabara
inapotenganisha magari yanayopanda na yanayoshuka
Kijana
huyo akielekea kwenye sehemu yake ili kuweza kuyapisha magari na baada
ya magari kusimama tena aliweza kuendelea kufanya kazi hizo za kusafisha
vioo vya magari.
PICHA NA PAMOJA BLOG
0 comments:
Post a Comment