Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akisalimiana
na wanafunzi wa Shule ya Msingi Boma mara baada ya kufunga mafunzo ya
sanaa kwa watoto 200 wa shule za msingi tano za wilaya ya Ilala jijini
Dar es salaam jana. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Baraza la Sanaa la
Taifa (BASATA), na kufadhiliwa na kampuni ya Msama Promotions.
Baadhi
ya watoto wa Shule za Msingi kutoka Wilaya ya Ilala wakionesha vipaji
vya kucheza ngoma wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya sanaa
yaliyoandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata),na kufadhiliwa na
Kampuni ya Msama Promotions . Jumla ya watoto 200 wamenufaika na mafunzo
hayo.
Mmoja wa wanafunzi akionesha mitindo ya mavazi.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Buguruni Visiwi wakionesha mitindo mbalimbali wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza katika hafla ya
kufunga mafunzo ya sanaa kwa watoto yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mafunzo hayo yaliandaliwa na Basata na kudhaminiwa na Kampuni ya Msama
Promotions. Kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza
na Ofisa Tawala wa Kampuni ya Msama Promotions, Hamis Mussa.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Godfrey Mngereza akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mtoto
Mariam Yusuf akisimulia hadithi wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya
sanaa kwa watoto wa shule za msiongi kutoka Manispaa ya Ilala.
Mtoto Mariam akionesha kipaji chake.
Watoto wakicheza maigizo.
Baadhi ya watoto wa Shule ya Msingi Uhuru Wasichana wakiwa katika hafla hio.
Msama akiagana na wanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru Wasichana.
DAR ES SALAAM, Tanzania
MKURUGENZI
wa Kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, Alex Msama
amepongeza hatua ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), kuanzisha mafunzo
maalumu kwa watoto wa shule za msingi.
Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati wa kufunga mafunzo maalumu
yanayolenga kuwajenga watoto katika fani ya sanaa na kushirikisha watoto wapatao 200 kutoka shule tano za wilaya ya Ilala, Msama alisema ni jambo zuri kuandaa vipaji vya kesho.
yanayolenga kuwajenga watoto katika fani ya sanaa na kushirikisha watoto wapatao 200 kutoka shule tano za wilaya ya Ilala, Msama alisema ni jambo zuri kuandaa vipaji vya kesho.
“Mafunzo
haya yataweza kuwajenga watoto wetu ambao ndio taifa la kesho, pia
kupunguza tatizo la watoto kujiingiza katika mambo mabaya kama matumizi
ya bangi, dawa za ulevya, hivyo kuwa mzigo na janga kwa taifa,” alisema
Msama.
Shule zilizonufaika na mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Msama kupitia
kampuni yake ya Msama Promotions, waratibu wa Matamasha ya Pasaka na Krismas, ni Buguruni Moto, Buguruni Visiwi, Ilala Boma, Uhuru Wasichana na Msimbazi.
kampuni yake ya Msama Promotions, waratibu wa Matamasha ya Pasaka na Krismas, ni Buguruni Moto, Buguruni Visiwi, Ilala Boma, Uhuru Wasichana na Msimbazi.
Aidha,
Msama alihimiza umuhimu wa somo la sanaa shuleni akitaka
lipewe msisitizo mkubwa katika kuandaa vijana bora ambao hata kama
wakifeli masomo mengine, wanaweza kuwa wasanii bora. “Somo hili la sanaa mashuleni lipewe uzito unaostaili kama masomo mengine kwa sababu, mtoto akifeli masomo mengine, fani ya sanaa yaweza kuwa msaada kwake,” alisema.
Msama aliwashauri pia Basata kuyapeleka mafunzo hayo hadi mikoani na
kupendekeza kwa hatua ya awali waanzie katika mikoa ya Pwani na Morogoro, akiamini kuna vipaji vingi vya sanaa.
kupendekeza kwa hatua ya awali waanzie katika mikoa ya Pwani na Morogoro, akiamini kuna vipaji vingi vya sanaa.
Naye
Kaimu Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza alisema mafunzo hayo
yaliyoanza Machi 1, wanafunzi walikuwa wakifanya mazoezi ya sanaa
katika fani utambaji, hadithi, ngoma za asili na maigizo katika maeneo
ya shule zao chini ya usimamizi wa walimu wao na waratibu kutoka Basata.
Mngereza alimshukuru mgeni rasmi Msama kwa kudhamini mafunzo hayo
akisema amefanya hivyo kwa kutambua umuhimu wa elimu ya sanaa katika maisha ya kila siku.
akisema amefanya hivyo kwa kutambua umuhimu wa elimu ya sanaa katika maisha ya kila siku.
“Msama ameonesha wazi kuwa yeye ni mdau na mfurukutwa wa sanaa,
aliyepania kuendeleza sekta ya utamaduni hasa sanaa kwa kuibua vipaji vya
watoto,” alisema.
aliyepania kuendeleza sekta ya utamaduni hasa sanaa kwa kuibua vipaji vya
watoto,” alisema.
0 comments:
Post a Comment