UNITED
REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
|
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA UMMA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo,
Jumapili, Machi 16, 2014, amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais Jacob Zuma wa
Afrika Kusini.
Ujumbe
huo wa Rais Zuma umewasilishwa kwa Rais Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje wa
Afrika Kusini, Mheshimiwa Maite Nkoana-Mashabane wakati mama huyo alipokutana
na kufanya mazungumzo na Rais Kikwete, Ikulu, Dar Es Salaam.
Mara
baada ya kuwasilisha ujumbe huo, viongozi hao wamejadili masuala yanayohusu
uhusiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini na masuala ya kikanda ambako nchi
zote mbili ni wanachama wa Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Mheshimiwa
Nkoana-Mashabane amendoka nchini mara baada ya kuwa amewasilisha ujumbe huo kwa
Rais Kikwete.
Imetolewa
na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
16
Machi,2013
0 comments:
Post a Comment