Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja( meza kuu
mbele) akisaini Mkataba wa Uwekezaji katika shughuli za Kilimo na
Ufugaji na Mwekezaji toka nchini Uturuki, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni
ya TARBIM LTD, Bw. Baddal Calikusu(wa kwanza toka kulia). Hafla fupi ya
utilianaji saini Mkataba huo umefanyika Machi 17, 2014 Makao Makuu ya
Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akibadilishana
Mkataba wa Uwekezaji katika shughuli za Kilimo na Ufugaji na Mwekezaji
toka Nchini Uturuki ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya TARBIM LTD.
Jeshi la Magereza kupitia Shirika lake la Magereza limetiliana saini
Mkataba huo ambao utatekelezwa katika Shamba la Magereza lililopo
Bagamoyo, Mkoani Pwani.

Mkurugenzi wa Kampuni ya TARBIM LTD(kulia mbele meza kuu) akiagana rasmi
na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kushoto
mbele meza kuu) mara baada ya hafla fupi ya utilianaji saini wa Mkataba
wa Uwekezaji katika shughuli za Kilimo na Mifugo ambapo Jeshi la
Magereza kupitia Shirika lake la Magereza litatekeleza miradi ya
Uzalishaji ya Kilimo na Ufugaji katika Shamba la Magereza lililopo
Bagamoyo, Mkoani Pwani kwa kushirikiana na Kampuni ya Mwekezaji ya
TARBIM LTD

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja(mbele
meza kuu) akitoa utambulisho wa Makamishna wa Jeshi la Magereza(waliopo
kushoto)kwa Mwekezaji wa shughuli za Kilimo na Ufugaji kabla ya
kutiliana saini Mkataba wa Uwekezaji wa masuala ya Kilimo na Ufugaji
katika Shamba la Magereza lililopo Bagamoyo, Mkoani Pwani.Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza
0 comments:
Post a Comment