Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Uongozi ni hali ya kushawishi kundi kutekeleza malengo fulani
waliyojiwekea. Kuna aina nyingi za uongozi kulingana na jinsi
wanavyopatikana.
Kuna uongozi wa kuteuliwa, kuchaguliwa kidemokrasia, kurithishwa (wafalme) na uongozi wa kipaji.
Hata hivyo, kumekuwa na tabia ya viongozi
kurithisha madaraka kwa ndugu na jamaa zao kwa lengo la kulinda masilahi
ya kifamilia yasipotee wakati hawapo madarakani.
Hali hiyo imejitokeza hivi karibuni ambapo Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kimejikuta kikirejesha watoto wa viongozi katika
nafasi za ubunge pale nafasi inapokuwa wazi, huku vyama vya upinzani
navyo vikiendelea na mtindo huo hali inayoonyesha uroho wa madaraka.
Hivi karibuni CCM kimemsimamisha Godfrey Mgimwa
ambaye ni mtoto wa Dk William Mgimwa aliyekuwa mbunge wa jimbo la
Kalenga kugombea ubunge katika jimbo hilo.
Godfrey Mgimwa alishinda kura za maoni kwa kupata
342, huku mshindi wa pili, Jackson Kiswaga akipata kura 170, watatu ni
Hafsa Mtasiwa aliyeambulia kura 42.
Katika uchaguzi huo, Mgimwa anapambana na Grace Tendega wa Chadema.
Akijibu shutuma kwamba, jimbo hilo linarithishwa
kifamilia, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye anasema chama
hicho hakiwezi kumnyima mwanachama yeyote haki ya kuwania kwa sababu tu
wazazi wake waliwahi kuwa viongozi.
“CCM haiwezi kumzuia Godfey kuwania eti kwa sababu
ni mtoto wa Dk Mgimwa (marehemu). Yeye ana haki ya kuwania kama watu
wengine tunachoangalia ni uwezo wake na hilo limeonyeshwa baada ya
wananchi wa Kalenga kumpa ushindi wa kishindo,” alisema.
Wakati joto la uchaguzi likishika kasi Kalenga,
jimbo la Chalinze mkoani Pwani nako amepitishwa mtoto wa Rais Jakaya
Kikwete, Ridhiwani. CCM imempitisha Ridhiwani baada ya kushida kwa kura
758, akifuatiwa na Wakili Imani Madega aliyepata kura 335.
Mbali na wagombea hao wapya, mwaka 2012 baada ya
kufariki aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha, Jeremiah Sumari ambaye pia
alikuwa mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki, CCM ilimsimamisha mwanaye,
Sioyi Sumari kugombea.
Hata hivyo mgombea wa Chadema, Joshua Nasari alishinda
Mbali na ubunge, mwaka 2000 chama hicho kilishamrithisha
madaraka ya urais Amani Abeid Karume mtoto wa mwasisi wa Taifa la
Zanzibar, Abeid Amani Karume.
Amani alikuwa rais wa sita wa Zanzibar, huku ndugu yake, Ali Karume naye akiiwania nafasi hiyo kwa muda mrefu bila mafanikio.
Hali hiyo ya kurithishana madaraka iwe kwa
kuteuliwa au kupendekezwa kugombewa haipo CCM pekee, bali hata kwa vyama
vya upinzani.
C hadema: Kwa muda mrefu kumekuwa na malalamiko
ya chini kwa chini juu ya mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye ni
mkwe wa mwasisi wa chama hicho, Edwin Mtei.
Mbowe amekuwa mwenyekiti wa chama hicho tangu mwaka 2004 alipogombea na kushinda akimrithi Bob Makani (marehemu).
Katika uchaguzi mkuu wa chama hicho wa 2009, wazee
wa chama hicho wakiongozwa na Mtei, walimzuia aliyekuwa Naibu Katibu
Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe kugombea nafasi hiyo kwa maelezo kuwa
hajakomaa, huku wakimtaka amwachie Mbowe amalizie kipindi chake cha
pili.
Mwaka huu, Chadema itafanya uchaguzi mkuu, lakini
haijaeleweka kama Mbowe ataendelea kugombea nafasi hiyo au atamwachia
mwingine.
Undugu katika Chadema umeonekana kushika kasi
katika nafasi za ubunge wa kuteuliwa ambapo ndugu wa kifamilia wa
viongozi wa juu wanaonekana kuteuliwa kuwa wabunge wa viti maalumu.
Lucy Owenya aliyepata ubunge wa viti maalumu kwa
kipindi cha pili sasa ni mtoto wa moja wa waasisi, kiongozi wa chama
hicho na mbunge wa Moshi mjini Philemon Ndesamburo.
Wengine ambao ni wabunge wa viti maalumu na ambao
ni ndugu wa karibu wa viongozi wa juu wa chama hicho ni pamoja na Grace
Kiwelu aliyedumu katika ubunge wa viti maalumu kwa vipindi vitatu,
ambaye ni mke wa mtoto wa Ndesamburo na Rose Kamili alikuwa mke wa
Katibu Mkuu Dk Wilbroad Slaa .
Undugu pia unatajwa kudhoofisha demokrasia ndani
ya vyama vya siasa ikiwamo UDP ambako mwenyekiti wake, John Momose
Cheyo na mdogo wake, Isaack Cheyo wamekaimishana uongozi wa chama hicho.
Chanzo;mwananchi
Chanzo;mwananchi
0 comments:
Post a Comment