Home » » Tanzania yaandaa mkutano wa kimataifa wa kupinga ujangili

Tanzania yaandaa mkutano wa kimataifa wa kupinga ujangili

 Waziri wa Maliasili na utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza na waandishi wa habari
 Wadau na Viongozi mbalimbali wa sekta ya Utalii nchini

 Mwakilishi Mkazi kutoka Shirika La Maendeleo La Kimataifa UNDP, Philippe Poinsot
 Waziri wa Maliasili na utalii, Lazaro Nyalandu (katikati) akitia saini makubaliano ya ushirikiano wa kuandaa mkutano wa wa wadau wa utalii, kushoto kwake ni Mwakilishi Mkazi kutoka Shirika La Maendeleo La Kimataifa UNDP, Philippe Poinsot na kulia ni Makamu Mwenyekiti  wa Shirika La Uhifadhi Wa Mazingira La Kimataifa La Nchini Marekani ICCF, Dk. Kaush Arha
Makamu Mwenyekiti  wa Shirika La Uhifadhi Wa Mazingira La Kimataifa La Nchini Marekani ICCF, Dk. Kaush Arha

Dotto Kahindi 

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii na Shirika La Uhifadhi Wa Mazingira La Kimataifa La Nchini Marekani (ICCF) kwa kushirikiana na Shirika La Maendeleo La Umoja wa Mataifa (UNDP) wameandaa mkutano mkubwa wa kupinga ujangili utakaofanyika nchini Tanzania Mei 9 hadi 10 mwaka huu.

Akitia saini makubaliano ya ushirikiano huo mapema jana Waziri wa Maliasili na utalii, Lazaro Nyalandu amesema kuwa mkutano huo unalenga kutoa wito kwa wadau mbalimbali wa uhifadhi na utalii juu ya njia stahiki za mapambano dhidi ya ujangili nchini Tanzania.

Alisema kupitia mkutano huo ambao utawakutanisha wadau wa uhifadhi wa maliasili na utalii kutoka kwenye mataifa mbalimbali ili kutoa na kujadili mapendekezo ya maksudi ya kukabiliana na ujangili nchini yatakayoisaidia Tanzania kukomesha ujangili huo.

Nyalandu amesema serikali ya Tanzania imekuwa ikifanya jitihada za kukabiliana na ujangili kwa kila hali lakini wameona kuna umuhimu mkubwa wa kushirikisha wadau na mashirika ya kitaifa na kimataifa katika kupafanikisha vita hivyo.

“Tanzania ni nchi ya pili duniani kwa kuwa na vivutio vya utalii na unaweza kuona ni kwa kiasi gani ni muhimu kuongeza kasi ya kupambana na majangili ambao wanalengo la kuharibu maliasili hizi adimu” alisema Nyalandu

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi kutoka Shirika La Maendeleo La Kimataifa UNDP, Philippe Poinsot alisema kuwa mkutano wa mwezi Mei unamantiki kubwa katika kukabiliana na ujangili nchini kwa kuwa utawakutanisha wadau muhimu katika masliasili na utalii.

Alisema mkutano huo hautaishia tu kujadlili changamaoto iliyopo katika ujangali nchini bali utakwenda mbali kwa kuangalia suluhisho la changamoto hizo ili kuiweka Tanzania huru na vitendo vya ujangili.

“Mkutano huu hautakuwa na maana kama tutaishia kujadili changamoto bila kubainisha njia za kuzitatua changamoto hizo” alisema Poinsot

Naye Makamu Mwenyekiti  wa Shirika La Uhifadhi Wa Mazingira La Kimataifa La Nchini Marekani ICCF, Dk. Kaush Arha alisema katika kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ya Tanzania katika kupambana na ujangili wameamua kutoa mchango wao kwa kushiriki mkutano huo ambao anaamini utafanikisha kupata mapendekezo muhimu katika kukabiliana na ujangili.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa